Na Boniface Wambura
MECHI
za kwanza za hatua ya tatu ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania
nafasi tatu za kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao zinachezwa
wikiendi hii kwenye viwanja vinne tofauti.
Mechi
za kesho (Jumamosi) ni kati ya Kariakoo ya Lindi na Friends Rangers ya
Dar es Salaam utakaochezwa katika Uwanja wa Ilulu mjini Lindi wakati
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi
kati ya wenyeji Kimondo SC na Njombe Mji.
Timu
za Machava FC ya Kilimanjaro na Stand United FC ya Shinyanga, Polisi
Jamii ya Mara na Katavi Warriors ya Katavi zilizokuwa zipambane kesho
mechi zao zimesogezwa mbele hadi keshokutwa (Jumapili). Mechi hizo
zimesogezwa kutokana na viwanja vya Ushirika mjini Moshi na Karume mjini
Musoma kuwa na shughuli nyingine za kijamii.
Hata
hivyo, TFF imesisitiza kuwa ikibainika kuwa viwanja hivyo havikutumika
kwa shughuli za kijamii siku hiyo ya Jumamosi, hatua kali zitachukuliwa
kwa wanachama wake (vyama vya mpira wa miguu vya mikoa husika).
Mechi
za marudiano za hatua hiyo ya tatu zitachezwa Juni 19 mwaka huu. Hatua
ya nne ya RCL itachezwa kati ya Juni 23 na 23 mwaka huu wakati mechi za
marudiano zitachezwa kati ya Juni 29 na 30 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment