Baadhi ya wachezaji vijana wa Simba |
KLABU ya soka ya Simba ambayo imekuwa ikijifua kwenye uwanja wa Kinesi kwa ajili ya ushiriki wa Kombe la Kagame, japo kulikuwa na tishio la kutokwenda kutokana na kutishwa na hali ya usalama mjini Darfur, Sudan kesho jioni itashuka dimbani kuumana na Golden Bush Fc katika pambano la kirafiki.
Pambano hilo litachezwa kwenye uwanja wa Kinesi, ambapo Golden Bush inayonolewa na nyota wa zamani wa Kagera Sugar, Shija Katina, imepania kutoa upinzani mkali kwa 'Mnyama' inayonolewa na kocha Abdallah Kibadeni 'King Mputa'.
Kwa mujibu wa Mlezi wa klabu ya Golden Bush, Onesmo Wazir 'Ticotico', ametoa taarifa kwamba kikosi chao kipo imara kwa pambano hilo la timu yao ya vijana kabla ya Jumapili asubuhi timu yao wa Veterani , Golden Bus veterans kushuka dimbani kupambana na Mburahati Veterani uwanja wa Chuo Kikuu.
Taarifa rasmi ya Ticotico inasomeka kama ifuatavyo:
Wadau,
Naomba nitoe taarifa kwamba weekend hii, Golden Bush FC wazee na vijana tutakuwa na ratiba kama ifuatavyo:
Kesho Jumamosi (Uwanja Kinesi jioni)
Vijana
wataingia uwanjani kumenyana na Wekundu wa Msimbazi (Simba sports
Club). Maandalizi ya game yamekamilika na Simba hatimaye wamekubali
kukabiliana na goldeb bush katika Uwanja wa Kinesi, timu imeandaliwa
vizuri kabisa na tunataka kutoa upinzani wa kufa mtu dhidi ya Simba ili
kuwakomesha na mpira wao wa magazetini. Game itaanza saa kumi na nusu
alasiri/jioni
Keshokutwa Jumapili (Uwanja wa chuo Kikuu asubuhi)
Wazee
wa kazi, wazee wa kuleta migogoro kwenye timu pinzani, wazee wanaotisha
dar es salaam watakuwa na game ya kirafiki dhidi ya Mburahati veterans.
Game hii itachezwa viwanja vya Chuo kikuu cha Dar es salaam, tumepeleka
hii game pale kwa maksudi ili Mwenyekiti wa chuo apime mwenyewe kama
timu yake inaweza kucheza na sisi au afuate utaratibu wa Survey Veterans
(yaani kugomea mchezo).
Baada
ya kusema hayo naomba sasa Mwenyekiti wa chuo ukubali ombi letu la
kucheza na Chuo veterans siku ya weekend inayofuata tarehe 22/06/2013.
Naomba kutoa hoja
Onesmo
No comments:
Post a Comment