STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, November 5, 2013

Man City dhidi ya wabaguzi wa rangi, Mashetani kuwavaa Wahispania

Yaya Toure alipokuwa akilalamikia ubaguzi kwa mwamuzi siku ya pambano lao la CSKA
Manchester United inamatumaini ya kutwaa kombe msimu huu huku vidole vyake ikivinyosha kwa Robin van Persie na Wayne Rooney ambao David Moyes anaamini kombinesheni yao ya ushambuliaji kwa sasa inatisha.
Mholanzi na Muingereza huyo Jumamosi walifunga mabao wakati United ikishinda 3-1 dhidi ya Fulham kwenye mechi ya ligi kuu, hizo zikiwa ni salamu kwa Real Sociedad ambayo watakutana nayo leo katika mchezo wa Kundi A wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hiyo ni mechi yao ya tatu wawili hao kufunga katika mchezo mmoja wakiwa chini ya Moyes, ambaye huo ni msimu wake wa kwanza baada ya kurithi mikoba ya Mscotland mwenzake, Alex Ferguson, huku kwa Van Persie hilo likiwa bao lake la sita msimu huu kwenye ligi kuu na Rooney likiwa la tano.
"Nadhani sasa kumbinesheni yao ni nzuri na wote wanatengenezeana mabao," Moyes alisema katika mkutano na waandishi wa habari.
 Nhodha wa United, Nemanja Vidic pia aliwanyoshea mikono washambuliaji hao wawili.
 "Kwa ujumla nilifurahishwa na Robin na Wayne," beki huyo wa kati raia wa Serbia aliiambia TV ya United, MUTV.
Katika hatua nyingine wapinzani wa Mashetani Wekundu kwenye Ligi Kuu ya England, Manchester City baada ya wiki mbili zilizopita mashabiki wa CSKA Moscow kumfanyia vitendo vya kibaguzi, Kiungo wa Manchester United, Yaya Toure, leo wabaguzi hao watakuwa na kibarua kigumu watakaposhuka Uwanja wa Etihad.
Timu hizo zitakuwatana katika mfululizo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo katika mechi nyingine ya Kundi D, Viktoria Plzen itakuwa mwenyeji wa Bayern Munich wakati Kundi A Shakhtar Donetsk ikiialika miamba mingine ya Ujerumani, Bayer Leverkusen.
Kwa upande wa Kundi C Paris St Germain itakuwa mwenyeji wa Anderlecht huku Olympiakos Piraeus ikiialika Benfica.
Kesho Ligi hiyo itaendelea kwa kuzikutanisha Basel vs Steaua Bucharest, Chelsea vs Schalke 04,
Borussia Dortmund vs Arsenal,
Napoli vs Olympique Marseille na
Zenit St Petersburg vs Porto.
Mechi zingine zitakuwa kati ya
Atletico Madrid vs Austria Vienna,
Ajax Amsterdam vs Celtic na Barcelona vs AC Milan.

No comments:

Post a Comment