
HABARI zilizotufikia muda huu zinasema kuwa Watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wamenaswa na jeshi la Polisi wakijiandaa kufanya tukio eneo la Mbagala-Dar es Salaam.
Taarifa hizo zinasema kuwa majambazi hao walinaswa wakiwa kwenye pikipiki yenye namba za usajili T 225 CQC aina ya Kapor baada ya kushtukiwa.
Inaelezwa wakora hao walinaswa wakiwa na silaha wakijiandaa kufanya uhalifu katika kituo cha kuuza mafuta cha Oilcom kilichopo Kongowe-Mbagala, jijini Dar!
Majambazi
hayo yametiwa mbaroni na askari polisi zaidi ya kumi waliokuwa
wamevalia nguo za kiraia wakiwa na magari aina ya Land Cruiser yenye
namba za usajili T 148 AEN na T 848 AGF!
Tukio hili limekuja siku moja baada ya jana jeshi hilo kuwanasa watu wengine wanaodaiwa kuwa majambazi kwenye kituo cha mabasi cha Ubungo wakijiandaa kufanya uhalifu.
No comments:
Post a Comment