STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, March 12, 2014

Yanga warejea toka Misri, Simba wawapa dole!

Yanga
WAKATI kikosi cha Yanga kilichotolewa kishujaa katika Ligi ya Mabingwa ya Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, kikirejea nchini kutoka Cairo, watani zao Simba wamewapongeza kwa kiwango cha soka walichoonyesha mbele ya watetezi wa michuano hiyo ya Afrika.
Yanga iling'olewa kwa mikwaju ya penati 4-3 na watetezi hao baada ya kukubali kipigo cha 1-0 katika dakika 90 na kulingana magoli baada ya mechi ya kwanza wenyewe kushinda nyumbani idadi kama hiyo iliwasili leo na kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Said Mecky Sadiq.
RC huyo aliapongeza wachezaji na viongozi wa Yanga kwa namna walivyoipigania Tanzania, ingawa bahati haikuwa yao huku akiwataka wanaowasakama wachezaji hasa Said Bahanuzi kuacha jambo hilo kwa madai hata mastaa duniani hukosa penati na bado wanapongezwa na wadau wao.
Katika hali isiyotarajiwa Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga amenukuliwa akiwapongeza watani zao kwa mchezo waliouonyesha ugenini licha ya kushindwa kufikia rekodi yao ya kuwang'oa watetezi wa taji la Afrika,
Kamwaga alisema kila mtu ameona watani zao walivyopigana ingawa hawakuwa na bahati ya kupenya hatua hiyo na Simba kama wadau wengine wa soka wanapongeza na kuwakarisha kwenye ligi kuu.

No comments:

Post a Comment