STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, March 12, 2014

Arsenal majanga, Ozil nje kwa majeraha

Arsenal's Mesut Ozil in action against Bayern Munich (AFP)
Mesut Ozil alipokuwa wakifanya mambo yake kabla ya kutolewa baada ya kuumia jana


HUENDA hii ikawa ni taarifa mbaya kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal ambao wanaugulia kutolewa kwa timu yao kwenye hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana, baada ya kudokezwa kuwa huedna wakamkosa kiungo wao mahiri, Mesut Ozil aliyeumia katika pambano hilo la usiku wa jana
Meneja Arsene Wenger amethibitisha kuwa watakosa huduma za kiungo huyo aliyeumia katika mechi hiyo ikiwa ni siku chache baada ya kurejea kwenye kiwango chake na kuivusha Arsenal kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA.
Mchezaji huyo wa bei mbaya kwa klabu hiyo aliyolewa wakati wa mapumziko wakati matokeo yakiwa 1-1 na kocha Wenger amesema hana hakika itamchukua muda gani nje ya dimba, ila amekiri hatamtumia kwenye mechi yao ya Jumapili dhidi ya mahasimu wao wa London Kaskazini, Tottenham Hotspur.
"Linaonekana ni tatizo kubwa," alisema kocha huyo na kuongeza; "Sijui nitamkosa kwa muda gani, ila nina hakika hatacheza mechi ya Jumapili dhidi ya Spurs."
"Tutamfanyia vipimo kesho (leo) ili kujua tatizo lake lipo kwa kiasi gani ina atakuwa nje kwa wiki kadhaa. Natumaini halitakuwa tatizo kubwa sana," aliongeza kocha huyo toka Ufaransa.

No comments:

Post a Comment