STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, March 12, 2014

Arsenal yang'oka, AC Milan aibu tupu Ligi ya Mabingwa Ulaya

Bastian SchweinsteigerAtletico Madrid's Diego Costa (R) celebrates with teammate Raul Garcia after scoring a goal against AC Milan during their Champions League last 16 second leg (Reuters)
Diego Costa akishangilia bao lake la Garcia

Jikaze wewe hii kazi ya kiume bana!
Atletico Madrid wakishangilia
Frank Ribery akichuana na wachezaji wa Arsenal
MABINGWA wa zamani wa Ulaya, AC Milan ya Italia imeyaaga michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kukung'utwa ugenini mabao 4-1 na Atletico Madrid ya Hispania, huku Arsenal ikitoka sare ya 1-1 ugenini lakini imekwama kutinga Robo Fainali  dhidi ya Bayern Munich.
Atletico ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Vicente Calderon iliifumua Milan na kutinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 5-1 kwani mechi ya kwanza nchini Italia ilishinda 1-0.
Wenyeji waliwashtukiza wageni wao kwa bao la mapema la dakika tatu tu lililofungwa na nyota wa timu hiyo Diego Costa kabla ya Kaka kuisawazishia Milan bao dakika ya 27.
Hata hivyo Atletico iliongeza bao la pili dakika ya 40 kupitia kwa Turan na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 2-1.
Kipindi cha pili kilikuwa cha wenyeji baada ya kuongeza mabao mengine katika dakika ya 70 lililofungwa na Raul Garcia na Diego Costa aliongeza jingine dakika tano kabla ya pambano kiumalizika.
Katika mechi nyingine iliyochezwa kwenye uwanja wa Allianz Arena, mjini Munich nchini Ujerumani, watetezi wa taji hilo, Bayern Munich waliiondosha tena mashindanoni Arsenal ya England baada ya kutoka nao sare ya 1-1.
Arsenal ilikwama kufuzu hatua ya 16 Bora kwa mwaka wa tano mfululizo baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 nyumbani kwao wiki mbili zilizopita na hivyo sare ya jana imewafanya waage michuano hiyo kwa jumla ya mabao 3-1.
Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Bastian Schweinsteiger katika dakika ya 54 kabla ya Lukas  Podolski kuisawazishia wageni dakika tatu baadaye.
Kivumbi cha ligi hiyo kitaendelea leo kwa mechi nyingine mbili Barcelona itakuwa nyumbani kuikaribisha Manchester City ambayo katika mechi yao ya kwanza waliifumua kwa mabao 2-0 na pambano jingine ni kati ya PSG ya Ufaransa dhidi ya Bayer Leverkusen walioitambia kwao mabao 4-0.

No comments:

Post a Comment