STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, March 12, 2014

Wenger amponda Arjen Robben kwa udanganyifu

Arsenal's Laurent Koscielny (right) fouls Bayern Munich's Arjen Robben in the penalty area (PA Photos)
Arjen Robben akiwa amenguka ndani ya eneo la penati la Arsenal mbele ya Laurent Koscielny
MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amemponda winga nyota wa Bayern Munich, Arjen Robben kwa madai ya udanganyifu wa kujirusha ili kushawishi marefa kuipa penati timu yake.
Mfaransa huyo alisema kuwa Robben licha ya kuwa bonge la mchezaji anayemkubali, lakini pia amemsifia kuwa ni hodari wa kujirusha baada ya jana kuhusika na tukio la kujirusha langoni mwa Arsenal ili kushawishi penati kama alivyofanya kwenye mechi ya awali mjini London, japo penati hiyo ilikoswa.
Katika tukio hilo la awali, Mholanzi huyo alisababisha kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny kutolewa nje ya dimba kwa kadi nyekundu kwa kile kilichoonekana kumchezea rafu mbaya Robben.
Jana winga huyo alirejea tena na kuipa timu yake penati dakika za lala salama ambayo ilipotezwa na Thomas Muller na kuinusuru Arsenal kuchezea kicha pili mfululizo kwa Bavarians hao ambao hata hivyo wamesonga mbele.
"Siwezi kupinga, Robben ni bonge la mchezaji, ila ni mjanja wa kulazimisha mambo kwa kupenda kwake kujirusha mbele ya mabeki ili aonekane kachezewa vibaya, haivutii," alisema Wenger baada ya mechi ya jana dhidi ya Bayern Munich, ambapo winga huyo alionekana kama kachezewa rafu na Laurent Koscielny.
Wenger alisema kama marefa wangekuwa wakimpa kadi ya njano, hadhani kama angerudia mchezo wake huo ambao alidai unapoteza mvuto wa soka kwani ni udanganyifu unaoziumiza timu nyingine wakati mwingine.

No comments:

Post a Comment