STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 2, 2014

MAUAJI YA KUTISHA NCHINI CHINA


KUNDI moja la watu waliojihami kwa visu limewauawa takriban watu 28 katika kituo kimoja cha treni kusini magharibi mwa mji wa Kunming, nchini China.
Kituo cha habari cha Xhinua kimesema kuwa zaidi ya watu mia moja walijeruhiwa.
Baadhi ya majeruhi katika shambulio hilo wakiwa hospitali. 
Mashahidi wamesema kuwa washambuliaji hao waliovalia nguo nyeusi,waliwavamia abiria waliokuwa wakingojea kuabiri treni na kuwakatakata huku wengine wakiwadunga visu wale walioshindwa kukimbia kwa kasi.
Miili ya watu waliouawa katika shambulio hilo.
Kulikuwa na takriban washambuliaji 10..Polisi waliwapiga risasi na kuwaua washambuliaji 5 huku wakiwasaka waliosalia. Shirika la habari la Xhinua limewalaumu watu wanaopigania kujitenga katika mkoa wa Shinjiang kwa tukio hilo.
Baadhi ya mizigo iliyoachwa eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment