STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 2, 2014

Yanga yaweka rekodi EAC kama Flambeau de l'Est na AS Kigali

Yanga
USHINDI wa bao 1-0 iliyopata dhidi ya watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri imeifanya klabu ya Yanga kuwa moja ya timu tatu pekee za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilizopata ushindi barani Afrika mwishoni mwa wiki.
Yanga walipata ushindi huo kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa ni mara yao ya kwanza kuifunga timu kutoka Misri na ukanda wa Afrika Kaskazini baada ya zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Timu nyingine za ukanda huo iliyotakata Afrika ni; Flambeau de l'Est ya Burundi iliyoiduwaza Cotonsport ya Cameroon katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuilaza bao 1-0 mjini Bunjumbura, huku AS Kigali ya Rwanda ikishinda pia nyumbani kwa bao 1-0 katika michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shendi ya Sudan Kusini.
Timu hizo tatu Yanga, Flambeau de l'Est na AS Kigali zinahitaji sare yoyote ugenini kuweza kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya michuano wanayoishiriki baadaye wiki hii.
Wawakilishi wengine wa jumuiya hiyo, Gor Mahia na AFC Leopards za Kenya zenyewe zilichezea vichapo katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.
Gor Mahia ilifungwa nyumbani na Esperance ya Tunisia katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mabao
3-2, huku Leopards wakinyukwa ugenini mabao 2-0 na Supersport ya Afrika Kusini.
Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, KCCA ya Uganda, walilazimisha sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi
ya Nkana Red Devil's ya Zambia na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika mechi ya
marudiano mjini Kampala.
Timu za ukanda wa Afrika Mashariki, zimekuwa haina matokeo mazuri kwenye michuano mikubwa
barani Afrika, lakini ushindi iliyopata Yanga, Flambeau de l'Est na As Kigali na sare ya KCCA ni dalili njema, ingawa Gor Mahia na AFC Leopards bado nazo zina nafasi ya kujiuliza wikiendi hii.

No comments:

Post a Comment