STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 2, 2014

Spurs, Aston Villa zashinda England

Roberto Soldado
Wachezaji wa Spurs wakipongezana baada ya kupata bao pekee dhidi ya Cardiff  City

Leandro Bacuna
TOTTENHAM Hotspur muda mfupi uliopita imepata ushindi kiduchu nyumbani dhidi ya Cardiff City, huku Aston Villa kupata ushindi wa kishindo nyumbani kwa kuifumua Norwich City kwa kuilaza mabao 4-1 katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England.
Roberto Saldado aliifungia Spurs bao pekee katika dakika ya 28 baada ya kutengenezewa pande zuri na Emmanuel Adebayor na kuifanya Spurs kujiimarisha kwenye nafasi ya tano ikiwa na pointi 53.
Aston Villa ikiwa uwanja wake wa nyumbani iliifumua Norwich City kwa mabao 4-1, ambapo wageni walitangulia kupata bao dakika ya tatu tu ya mchezo iliyofungwa na Hoolahan kabla ya Christian Benteke akiisawazishia bao dakika ya 25 na kuongeza jingine dakika moja baadaye na Bacuna aliionheza bao la tatu na Sebastian Bassong alijifunga bao katika dakika ya 41 na kuifanya wenyeji kupata ushindi huo mnono.
Katika mechi nyingine, Swansea City ilishindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Crystal Palace.No comments:

Post a Comment