STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 2, 2014

Ashanti Utd, Kagera Sugar zatakata, Prisons yabanwa na Mgambo JKT

Ashanti United iliyoifumua Rhino Rangers
Kagera Sugar iliyoitandika JKT Ruvu
WAUZA Mitumba wa Ilala, Ashanti United imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya 'vibonde' wenzao Rhino Rangers ya Tabora, ushindi kama iliyopata Kagera Sugar nyumbani kwao mjini Bukoba dhidi ya JKT Ruvu, huku Prisons na Mgambo zikigawana pointi Mbeya.
Mechi hizo tatu ni kati ya nne zilizochezwa leo Jumapili, ambapo kwenye uwanja wa Chamazi, Ashanti ilipata ushindi wake wa pili kwenye duru ili la pili baada ya nyota wa zamani wa Yanga, Abubakar Mtiro kufunga bao hilo pekee lililoipa Ashanti pointi tatu na kuzidi kuiweka pabaya Rhino katika janga lake la kushuka daraja.
Nayo timu ya Kagera Sugar kwenye uwanja wake wa Kaitaba, iliizima JKT Ruvu iliyoshuka dimbani hapo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa kushtukiza dhidi ya Simba wiki iliyopita kwa kuilaza bao 1-0.
Bao hilo pekee la mchezo huo lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Themi Felix katika dakika ya 43 na kuifanya Kagera kujizatiti kwenye nafasi ya tano nyuma ya Simba, huku JKT ikisaliwa na pointi zao 22.
Katika pambano jingine la ligi hiyo leo lililochezwa uwanja wa Sokoine, Mbeya baada ya Mgambo JKT kuwabana wenyeji wao Prisons na kutoka sare ya 1-1.
Mgambo walitangulia kufunga bao lililodumu hadi wakati wa mapumziko kabla ya wenyeji kuchomoa kupitia kwa Laurian Mpalile katika kipindi cha pili na kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote kwenye duru la pili na wiki ijayo itakabiliwa na Simba.

No comments:

Post a Comment