STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 2, 2014

Ronaldo aiokoa Real Madrid isife kwa Atletico

Cristiano Ronaldo
Ronaldo akishangilia bao lao la kusawazisha dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid leo
BAO la dakika ya 82 lililofungwa na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kwa pasi ya Gareth Bale imeiokoa vinara hao wa Ligi Kuu ya Hispania kufa mbele ya mahasimu wao wa jiji la Madrid, Atletico Madrid na kulazimisha sare ya mabao 2-2.
Karim Benzema alitangulia kuifungia Real iliyokuwa uwanja wa ugenini dhidi ya Atletico baada ya kumalizia mpira wa Angel di Maria, lakini wenyeji walisawazisha dakika ya 28 kupitia kwa Koke kabla ya Gabi kuongeza la pili sekundu chache timu hazijaenda mapumziko.
Dakika nane kabla ya pambano hilo lililokuwa kali kumalizika Ronaldo aliifungia timu yake bao la kusawazisha na kuifanya iendelea kusalia kileleni ikiwa na pointi 64 huku wapinzani wao wakikwea hadi nafasi ya pili ila watakaa kwa muda iwao Barcelona itashinda mechi yake itakayochezwa baadaye dhidi ya Almeria.
Katika mechi nyingine zilizochezwa leo Villarreal ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Real Betis.

No comments:

Post a Comment