WAKATI sakata la Emmanuel Okwi hata halijapoa, uongozi wa Yanga upo kwenye msukosuko mwingine baada ya viongozi wa klabu ya FC Lupopo ya DR Congo kutua jijini na kudai kudhulumiwa fedha na klabu hiyo kupitia usajili wa Muyu Twite.
Mmoja wa viongozi wa FC Lupopo, amesema Yanga walitakiwa kulipa dola 15,000 kama wamemuongezea mkataba Twite.
"Lakini hawajafanya hivyo na nimekuja hapa viongozi wao Seif (Magari) na Abdallah (Bin Kleb) hawataki kulimaliza hili suala.
"Mwanzo walisema hawataki maneno na sisi lakini mkataba unaonyesha mchezaji ni wetu na anacheza kwao kwa mkopo tu.
"Kama waliona wanataka kuongeza mkataba lazima watulipe, tumewasiliana na chama chetu cha soka, ndiyo maana nimekuja hapa.
"Lakini
naona wanatuzungusha, tutasonga mbele hadi Fifa," alisema akisisitiza
amefika hadi TFF lakini mambo yanaonekana ni magumu.
Bin Kleb alinukuliwa na kituo kimoja cha redio kuwa atatoa ufafanuzi mara baada ya kutua Dar kwani alikuwa safarini.
No comments:
Post a Comment