MENEJA wa klabu ya
Liverpool, Brendan Rodgers amesema kuwa majeruhi ya Daniel Sturridge
yangeweza kuepukika na Chama cha Soka cha Uingereza kinapaswa kuwaepusha
wachezaji na majeruhi pindi wawapo katika majukumu ya
kimataifa.
Mshambuliaji huyo alicheza kwa dakika 89 wakati Uingereza
ikishinda bao 1-0 dhidi ya Norway katika Uwanja wa Wembley Jumatano
iliyopita kabla ya kurejea tena mazoezini saa 36 baadae na kupata
majeruhi akiwa mazoezini.
Sturridge, 25 alikosa
mchezo ambao Uingereza iliibugiza mabao 2-0 Uswisi katika mchezo wa
kufuzu michuano ya Ulaya Jumatatu kutokana na majeruhi hayo na sasa
anatarajiwa kukaa nje kwa wiki mbili zaidi.
Rodgers amesema
wamesikitishwa sana kutokana kazi kubwa aliyofanya wakati wa maandalizi
ya msimu kwani wanadhani majeruhi aliyopata yalikuwa yanaepukika kama
wahusika wangekuwa makini.
Liverpool itajitupa uwanjani Jumamosi hii
kukwaana na Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment