Mgeni rasmi wa mahafali ya Shule ya Brain Trust, Richard Mngomo alitoa nasaha zake jioni ya leo |
Wahitimu wakionyesha umahiri wao wa kuimba ngonjera |
Wahitimu wakielekea eneo la shughuli ya kuagwa kwao kwa kuhitimu darasa la saba |
Mkuu wa Shule ya Msingi, Nervin Marandu akitoa natoa nasaha zake |
Wahitimu wakiingia uwanjani kuonyesha umahiri wao |
Wakiimba |
Samuel Robert akiwaongoza wahitimu wenzake kuonyesha umahiri wa kuimba ngonjera |
Skauti wakionyesha umahiri wao mbele ya meza kuu |
Mericiana Ronald akianza kuonyesha umahiri wake wa kucheza muziki |
Acha kama Aisha Madinda! Mericiana akiendelea kuangusha rhumba |
Mkuu wa Shule ya Msingi, Nervin Marandu akisoma wasifu wa shule hiyo katika mahafali hayo pembeni yake ni mmoja wa walimu wa shule ya Brain Trust |
Immaculatha Justine Limonga akipokea cheti chake cha kuhitimu Darasa la Saba toka kwa mgeni rasmi |
Aidha wazazi wamesisitizwa kuhakikisha wanapambana na kusaidia kuwaendeleza watoto wao kwa masomo ya sekondari badala ya kuridhika na Elimu ya Msingi wanaomaliza watoto wao.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Shule ya Brain Trust, Irene Makinda wakati wa mahafari ya wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo yaliyofanyika jioni ya leo.
Makinda alisema wahitimu wa darasa la saba wanachangamoto kubwa katika kipindi chao cha kusubiri matokeo ya mitihani yao kwani wanakutana na na makundi ya watu tofauti, hivyo wawe makini.
Alisema ni vyema wazazi wakawaunganisha watoto wao na masomo maalum ya kujiandaa kujiunga sekondari (Pre form One) ili kuendeleza kuzifanya akili zao zichemke na kuepushiwa kuingia kwenye maovu.
"Hapa shuleni tunapokea wanafunzi kwa masomo hayo hivyo wazazi wasizembee wawalete watoto na pia shule yetu ina masomo ya sekondari hivyo wanafunzi wanaweza kuendelea hapa hapa," alisema.
Naye mgeni rasmi wa sherehe hizo zilizofanyika Yombo Vituka, Richard Mgomo wa Tanzania Printers, alisema wahitimu hao wa la saba wasidhani wameshamaliza kazi badala yake wajipange zaidi kimasomo.
"Kazi haijaisha, miaka saba mmepambana na kufanikiwa kufika mlipofikia, tunawapongeza, lakini kazi haijaisha kuna mtihani mkubwa zaidi mbeleni hivyo mjipange. Msiwangushe wazazi na walezi," alisema.
Mgomo, alisema ni wajibu wa wazazi na walezi kuwaendeleza watoto wao kwa masomo ya sekondari na nafasi hizo zikipatikana wanafunzi hao wasiwaangushe wazazi na walezi badala yake wajibidiishe zaidi.
Kabla ya mgeni rasmi huyo kuzungumza, Mkuu wa Shule ya Msingi Nervin Marandu alisoma historia fupi ya shule hiyo na kusema ilianzishwa Sept Mosi, 1998 ikiwa na wanafunzi 48 tu.
Hata hivyo alisema mpaka sasa shule hiyo ya msingi ina wanafunzi wapatao 850 na kusisitiza shule yao haibagui wanafunzi wa kuwapokea na kujivunia mafanikio inayopata kila mwaka tangu ianzishwe.
Katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali wakiwamo walimu wa shule za jirani na wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo kulipambwa na burudani toka kwa wanafunzi.
Miongoni mwa burudani hiyo ni mwanafunzi wa shule ya chekechea ya shule hiyo ya Brain Trush Mericiana Ronald aliyeonyesha kipaji cha kucheza muziki na kutuzwa maelfu ya fedha na waliokunwa naye.
No comments:
Post a Comment