Arsenal walipotungulia mapema mabao kabla ya kuyarejesha |
Alexis Sanchez (kushoto) akipongezwa kwa kufunga bao la kuongoza la Arsenal |
Cesc Fabregas akishangilia bao lake wakati Chelsea wakishinda ugenini |
Southampton wakishangilia karamu yao ya mabao |
Kun Aguero akishangilia moja ya mabao yake manne mapema leo walipoiua Spurs |
Welbeck aliyekuwa hapewi umuhimu wowote katika kikosi cha Manchester United na hivyo kuuzwa kwa Arsenal, alifunga bao hilo dakika za nyongeza kabla ya pambano kumalizika na kumpa nafuu meneja wake, Arsene Wenger.
Mshambuliaji huyo nyota wa England alifunga bao hilo akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Alexis Sanchez, ambaye alianza kuwafungia wenyeji bao dakika ya 13 kwa kumalizia kazi ya Per Martesacker.
Wageni walifunga mabao yao katika dakika ya 17 kupitia Mohammed Diamé kisha kuongeza la pili dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza kupitia kwa Abel Hernandez.
Katika mechi ya mapema leo, Sergio 'kun' Aguero aliisambaratisha Tottenham Hotspur waliowafuata nyumbani kwenye uwanja wa Etihad baa da ya kufunga mabao manne wakati wakiwazisha vijogoo hao wa London ya Kaskazini kwa mabao 4-1. Mabao mawili yakiwa kwa mikwaju ya Penati.
Nayo Southampton ikiwa nyumbani iliwasambatarisha Sunderland kwa kuwafunga mabao 8-0 ikiwa ni rekodi ya kipigo kikubwa katika msimu huu wa ligi ya England, huku Burnley ikiwa nyumbani ilifumuliwa mabao 3-1 na West Ham United na Everton walishinda nyumbani kwa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa.
Ushindi wa Southmpton umeifanya timu hiyo kufikia rekodi mojawapo ya mechi iliyokuwa na ushindi mnono ikienda sambamba na mechi nyingine tano tangu Ligi Kuu ilipoanza kutumika rasmi 1992 toka daraja la kwanza nchini humo..
Mechi nyingine za awali ni;
Manchester United 9-0 Ipswich, March 1995
Newcastle United 8-0 Sheffield Wednesday, September 1999
Tottenham Hotspur 9-1 Wigan Athletic, November 2009
Chelsea 8-0 Wigan Athletic, May 2010
Chelsea 8-0 Aston Villa, December 2012
Southampton 8-0 Sunderland, October 2014
No comments:
Post a Comment