VINARA wa Ligi Kuu ya England, Chelsea wataelekea kwa wapinzani wao jijini London Crystal Palace
Jumamosi wakilenga kupanua mwanya wa alama tano walioweka kileleni mwa
Ligi hiyo baada ya mapumziko ya kimataifa.
Palace walishangaza Chelsea, na klabu nyingine katika ligi, kwa kushinda
dhidi ya Chelsea msimu uliopita na nahodha wa Blues John Terry
amepuuzia mbali madai kwamba tayari mshindi wa ligi msimu huu
amejulikana.
“Ni wazi (kwamba kinyang’anyiro cha ligi) hakijaisha,” amesema Mourinho.
“Klabu nyingine zimejipata katika nafasi kama hii. Ni vyema kuongoza lakini ukiwa juu, kila mtu hutaka kukuangusha.
“Hilo ndilo jambo zuri kuhusu Ligi ya Premia na ndio maana kila mtu
huipenda. Timu zinalenga kutushambulia kwa sababu tuko juu na twacheza
vyema.”
Mabingwa watetezi Manchester City, walio wa pili kwa sasa, watakuwa
nyumbani dhidi ya Tottenham Hotspur na kiungo wa kati anayeichezea City kwa
mkopo Frank Lampard amewaambia wachezaji wenzake wajihadhari dhidi ya
Spur ambao wameanza kuamka.
“Huenda wanapitia kipindi cha mpito lakini nilifurahishwa sana na
meneja wao (Mauricio Pochettino) alipokuwa Southampton na ikiwa anaweza
kufanya hayo Tottenham, ambao bila shaka wana vipaji kwenye kikosi chao,
watafana. Ni timu nzuri sana.”
No comments:
Post a Comment