STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 18, 2014

SIMBA, YANGA MWISHO WA TAMBO LEO TAIFA

Simba
Yanga
http://2.bp.blogspot.com/-Be1qKCOuplk/UZcH0msefcI/AAAAAAAAGzU/gRe7zlSlB1w/s1600/katuni_watani.jpg
Katuni ya Chris Katembo nayo inazungumza je nani ataibuka mbabe leo Taifa?
BAADA ya tambo, kejeli na majigambo ya muda mrefu baina ya Simba na Yanga, hatma yote inatarajiwa kufahamika leo baada ya pambano lao litakalofanyika kwenye uwanja wa Taifa.
Simba na Yanga zinakutana katika pambano la 78 la Ligi Kuu tangu mwaka 1965, huku Yanga wakiwa wababe wa Simba kwa kushinda mara 29 dhidi ya 22 za watani zao wanaotokea kambini nchini Afrika Kusini.
Timu hizo zinakutana leo kwenye dimba hilo huku Simba wakionekana wachovu zaidi kulinganisha na Yanga msimu huu wakikamata nafasi ya 10 baada ya mechi za raundi tatu, wakati wapinzani wao wakiwa nafasi ya tatu wakitofautiana kwa pointi tatu.
Simba haijashinda pambano lolote kati ya 9 iliyochezwa kumalizia msimu uliopita na katika mechi za msimu huu, zaidi ya kuambulia sare tu.
Hata hivyo pambnano la watani huwa haliamuliwi kwa kuangalia rekodi kama hizo, kwani lolote huweza kutokea na kushangaza wale wanaotabiri labda kwa kuangalia udhaifu wa timu.
Mashabiki wa Yanga kwa sasa ni kama wanashangilia ushindi dhidi ya watani zao, lakini soka ni baada ya dakika 90 kwani lolote linaweza kutokea na kushangaa Simba wanaoonekana wanyonge kuibuka na ushindi dhidi ya watani zao.
Yanga inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kutokana na matokeo waliyoyapata kwenye michezo mitatu ya kwanza ya ligi kuu ya Bara ukilinganisha na sare tatu mfululizo za mtani Simba.
Yanga iliyoshinda michezo miwili, ina ponti tatu zaidi ya Simba kutokana na kufungwa na viongozi wa ligi Mtibwa katika mechi ya ufunguzi wa msimu.
Tayari makocha wa timu zote mbili wamekuwa wakitoa kauli tofauti kwa wiki kadhaa kuonyesha namna pambano hilo lisivyotabirika kirahisi.
Marcio Maximo amekuwa akisisitiza kuwa mashabiki waende uwanjani kuona kitakachotokea, bila kuweka bayana kama ana hakika Yanga kushinda ila anasisistiza kuwa wamejiandaa vya kutosha, wakati Patrick Phiri  ametadharisha na kusema ni mchezo huo utakuwa wa aina yake.
"Wenzetu wana matokeo mazuri zaidi yetu kwa kuwa wameshinda michezo miwili mfululizo laikini hilo haliwapi uhakika wa ushindi," alinukuliwa Phiri.
Phiri alisema anajua mapungufu ya wapinzani wao na kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo huku 'akiita' mashabiki kujaa kwa wingi uwanjani.
"Mashabiki (wa Simba) wasiwe na wasiwasi... tumejipanga vizuri kwa mchezo huu na kambi yetu ya Afrika Kusini imetusaidia.Tutapambana kupata ushindi.," alisema.
Kwa matokeo ya hivi karibuni, Simba tangu walipoifunga Yanga mabao 5-0 katika mechi ya kufungia msimu wa 2011-2012 haijashinda tena zaidi ya kuambulia sare na kuchapwa kama ilivyokuwa ligi ya kufungia msimu wa 2012-2013 walipolala mabao 2-0.
Timu hizo zinakutana huku kila moja ikiwa na idadi kubwa ya majeruhi ambao huenda wakakosekana uwanjani.
Simba ina uhakika wa kumkosa golikipa wake Hussein Sharif 'Casillas' huku pia mlinda mlango namba moja, Ivo Mapunda akiwa na uwezekano mdogo wa kuanza hivyo golikipa yosso Manyika Peter anatarajiwa kuanza golini.
Kwa upande wa Yanga, huenda ikamkosa kiungo wao nyota Haruna Niyonzima aliyeumia enka kwenye mazoezi ya timu hiyo wakati nahodha Nadir Haroub 'Canavaro' ambaye aliumia Jumapili akiwa na kikosi cha timu ya taifa na kushonwa nyuzi tatu ataangaliwa afya yake mpaka muda mfupi kabla ya mechi.
Katika mbili za msimu uliopita, timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya mechi ya awali kuisha kwa sare ya 3-3 na waliporudiana Aprili mwaka huu walifungana bao 1-1, Yanga wakilazimika kuchomoa 'usiku' kwa bao ya Simon Msuva, kama watani zao walivyochimoa mabao matatu katika ligi ya duru la kwanza.

No comments:

Post a Comment