STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 18, 2014

Gallas atundika galuga kimataifa

http://purelyfootball.com/wp-content/uploads/2014/08/1756906_201007087783881-1.jpg 
BEKI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, aliyewahi kutamba na klabu za Arsenal na Tottenham Hotspur, William Gallas ametangaza kustaafu soka rasmi baada ya kupita miaka 19 akicheza mchezo huo. 
Gallas mwenye umri wa miaka 37 amesema alikuwa akijiambia mwenyewe kwamba anaweza kuendelea lakini anadhani wakati umefika sasa wa kuamua kutundika daruga. 
Mkongwe huyo ambaye alianza rasmi soka lake katika klabu ya Caen mwaka 1995, aemcheza mechi 84 za kimataifa akiwa na Ufaransa na kufunga mabao matano likiwemo bao la utata katika ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa mtoano dhidi ya Ireland uliowapa nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2010. 
Gallas pia alicheza katika Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani ambapo Ufaransa ilifungwa na Italia kwa changamoto ya mikwaju ya penati. 
Baada ya kuitumikia klabu ya Olympique Marseille kuanzia mwaka 1997 mpaka 2001, Gallas alihamia Chelsea ambako alishinda mataji ya Ligi Kuu mwaka 2005 na 2006 na kujiunga na Arsenal msimu uliofuata kabla ya kuhamia Tottenham Hotspurs mwaka 2010. 
Octoba mwaka jana Gallas alisaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Perth Glory inayoshiriki Ligi Kuu nchini Australia maarufu kama A-League.

No comments:

Post a Comment