STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, November 11, 2014

Rasmi, michuano yaota mbawa 2014

http://cecafafootball.org/wp-content/uploads/2014/07/cecafa-2013-winners-kenya-Harambee-stars.jpg
Kenya wataendelea kubaki na taji lao la Chalenji
BAADA ya Ethiopia kuchomoa uenyeji wa michuiano ya Kombe la Chalenji 2014 na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, CECAFA kuiomba Sudan kuokoa jahazi, imethibitika safari hii haitakuwapo.
CECAFA imekwama kupata mwenyeji mpya baada ya Sudan nao kukataa ombi hilo.
Michuano hiyo ilitarajiwa kuanza Novemba 24 hadi Desemba 9, mwaka huu huko Ethiopia bingwa mtetezi akiwa ni Kenya.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka vya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Nicholas Musonye, alisema baada ya Ethiopia kujitoa, imekuwa ngumu kupata nchi mbadala ya kuandaa michuano kwa haraka.
“Hatukupenda, lakini imeshindikana kabisa, tulifanya kila juhudi lakini mambo yamekuwa ni magumu,” alisema Musonye.
Alisema  imekuwa ngumu kupata wadhamini pia kwani waandaaji walijitoa dakika za mwisho, hali iliyowachanganya.

No comments:

Post a Comment