STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, November 11, 2014

Hakunaga kama Cristiano Ronaldo Hispania

Ronaldo na moja ya Di Stephano

Ronaldo na tuzo zake
Akikabidhiwa tuzo ya Pichichi na Rais wa Atletico Madrid

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amezidi kung’ara baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya. Mfungaji Bora wa La Liga 'Pichichi' sambamba na ile ya Mchezaji Bora wa La Liga maarufu kwa jina la Di Stefano ikiwa ni mara ya tatu mfululizo tangu mwaka 2011 alipompoka mshindani wake kwa sasa dunia, Lionel Messi aliyekuwa akiishikilia kwa miaka miwili mfululizo pia.

Tuzo hizo alikabidhiwa na Rais wa Atletico Madrid Enrique Corezo, huku akisema ilikuewa huzuni kwa Alfredo Di Stefano kutukuwepo katika makabidhiano ya tuzo hiyo. Gwiji hilo la Real Madrid alifariki Julai mwaka huu akiwa na miaka 88.


WASHINDI:
TUZO YA PICHICHI
2009-10 Lionel Messi
2010-11 Cristiano Ronaldo 
2011-12 Lionel Messi
2012-13 Lionel Messi
2013-14 Cristiano Ronaldo 

TUZO YA DI STEFANO:
2009-10 Lionel Messi
2010-11 Lionel Messi
2011-12 Cristiano Ronaldo
2012-13 Cristiano Ronaldo
2013-14 Cristiano Ronaldo  

No comments:

Post a Comment