STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, November 11, 2014

Taifa Stars yapaa kwenda Afrika Kusini

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/07/team-stars-1.jpg
Wakali wa Tanzania, Taifa Stars
KIKOSI cha timu ya taifa, Taifa Stars, kimeondoka alfajiri ya leo kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kambi ya siku chache kabla ya kwenda kuvaana na Swaziland katika pambano la kirafiki la kimataifa linalotambuliwa na Shirikisho la Soka Dunia, FIFA litakalochezwa Novemba 16 mjini Mbabane nchini humo.
Kikosi cha wachezaji 24, benchi la ufundi na viongozi wengine wameambatana na timu hiyo kwa ajili ya kuhakikisha wanaendeleza rekodi nzuri dhidi ya Swaziland.
Stars mara ya mwisho kwenye mechi ya kimataifa waliifumua Benin mabao 4-1 uwanja wa Taifa na kuifanya timu hiyo ipae kwenye orodha ya viwango vya kimataifa vya soka vya FIFA.
Hata hivyo timu hiyo imekuwa na matokeo mabaya nje ya nchi kulingananisha ikiwa nyumbani kwani kabla ya kuvaana na Benin ilitoka kunyukwa mabao 2-0 na Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa mjini Bunjumbura.

No comments:

Post a Comment