STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, November 11, 2014

TCRA, Wanablogu kutetea asubuhi hii


MAMLAKA ya Mawasiliano nchini Tanzania, TCRA, asubuhi hii inatarajiwa kuteta na wamiliki wa mitandao ya kijamii ili kupeana miongozo kuelekea chaguzi zilizopo mbeleni.
Mkutano huo wa pamoja unatarajiwa kuanza saa 3 asubuhi kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam ambapo kwa mujibu wa 'bango' la TCRA lengo kuu ni kupeana muongozo wa kuandika taarifa za uchaguzi wa serikali za mitaa na ule wa mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.
Hata hivyo mbali na hilo, pia mkutano huo utatoa muongozo kwa wanablogu mingine juu ya kuzingatia maadili na miiko ya taaluma ya mawasiliano.
Kwa kipindi kirefu baadhi ya mitandao na blogu zimekuwa zikiweka taarifa au picha zinazokiuka maadili ya taaluma pamoja na miiko na desturi za kitanzania.
Nini kitakachojadiliwa na kuamuliwa, MICHARAZO itawajuza wasomaji wake bila ya shaka!

No comments:

Post a Comment