STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, November 11, 2014

Edin Dzeko azidi kuipa presha Man City

http://i4.mirror.co.uk/incoming/article2937913.ece/alternates/s615/Leicester-City-v-Manchester-City.jpgMSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester City, Edin Dzeko yupo katika hatihati ya kukosa pambano la nchi yake Bosnia-Herzegovina dhidi ya Israel kuwania kufuzu Fainali za Ulaya kutokana na kupata jeraha akiwa na timu hiyo ya taifa.
Mfumania nyavu huyo aliumia vibaya msuli wa kigimbi katika mguu wake wa kulia na Daktari wa timu ya taifa ya Bosnia-Herzegovina Reuf Karabeg amesema Dzeko, 28 anatarajiwa kukosa mchezo huo.
Karabeg alikaririwa akidai kuwa nyota huyo ameumia vibaya na atahitaji matibabu ambayo yatachukua muda mpaka kuja kupona.
Dzeko amefunga mabao manne katika mechi 17 katika kikosi cha City msimu huu lakini mpaka sasa ameshacheza mechi nane bila kufumania nyavu na kuumia kwake kutazidi kumtia tumbo joto kocha Manuel Pellegrini kutokana na kikosi cha timu yake kusuasua katika Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa mguu ndani mguu nje kutupwa mashindanoni.

Make Money at : http://bit.ly/best_tips

No comments:

Post a Comment