WATU
wapatao 48 wameuwawa katika shambulizi la bomu la kujitoa muhanga
katika shule moja huko kaskazini mashariki mwa Nigeria wengi wao wakiwa
wanafunzi.Mlipuko huo ulitokea jana Jumatatu katika mji wa Potiskum katika jimbo la Yobe wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa shule katika shule mioja ya sekondari ya serikali.
Wafanyakazi wa huduma wanasema watu wapatao 79 walijeruhiwa katika mlipuko huo , wengi wao wameumizwa vibaya . Magaidi wanasema mlipuaji huyo alivaa kama mwanafunzi. VOA
No comments:
Post a Comment