STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, November 11, 2014

Oscar aongezwa miaka 5 zaidi Darajani

Oscar
KLABU ya Chelsea imetangaza kumuongeza mkataba mpya wa miaka mitano kiungo wake mahiri Oscar. Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Chelsea toka alipojiunga nao akitokea klabu ya Internacional ya Brazil mwaka 2012.
Oscar, 23 amecheza mechi 15 na kufunga mabao manne katika mashindano yote msimu huu akiwa na Chelsea ambao hawajafungwa mpaka sasa.
Nyota huyo aliuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa anafurahi kusaini mkataba mpya kwani anafurahia kuitumikia Chelsea na kuishi nchini Uingereza.
Sasa Oscar ambaye ameitumikia Brazil mechi 40 na kufunga mabao 11, ataendelea kuwepo Stamford Bridge mpaka mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment