STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, November 11, 2014

Super Nyamwela amaliza Yangele

http://2.bp.blogspot.com/-RX3vTlkMHoc/UaW3K4F8znI/AAAAAAAAxNs/5mT7YRQLCUQ/s1600/Nyamwela+2.jpgDANSA kiongozi wa bendi ya Extra Bongo, Hassan Mussa 'Super 'Nyawela' amekamilisha 'audio' na video ya wimbo wake mpya uitwao 'Yangele Yangele' anaojiandaa kuutambulisha kwa mashabiki wakati wowote kuanza sasa.
Akizungumza na MICHARAZO jana, Nyamwela alisema wimbo huo umetengezwa kwenye studio za C9 Records  na vuideo yake imefanywa na Mkenya anayefahamika kwa jina la Yfeel.
Nyamwela alisema amechelewa kuitambulisha 'ngoma' yake hiyo kutokana na kuwa kwenye majonzi mazito ya kuondokewa na mama Mlezi wao, Mama Shuu, aliyekuwa Mke wa Mkurugenzi wa bendi yao, Ally Choki.
"Tumetoka kumaliza 40 ya Mama Shuu jana (juzi), tuliamua kupumzika kabisa masuala ya muziki kuomboleza kifo cha mama yetu na sasa tumerejea upya, nikiwataka mashabiki wangu wajiandae kuipokea kazi yangu mpya ya 'Yangele Yangele' ambayo imekamilika 'audio' na video yake," alisema Nyamwela.
Kabla ya kazi hiyo, dansa huyo wa zamani wa bendi ya African Star, alikuwa akitamba na nyuimbo kama 'Duvele Duvele', 'Tumechete', Maneno Maneno' na nyingine zilizokuwa katika albamu zake mbili za awali za 'Master of the Tample' na 'Afrika Kilomondo'.

No comments:

Post a Comment