![]() |
| Michael Olunga |
| Olunga (kulia) alipoikimbiza Yanga katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Kagame ambapo alifunga moja kuisaidia Gor Mahia kushinda 2-1 |
Olunga alifunga mabao hayo katika kipindi cha pili na kuiwezesha Gor Mahia kuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza robo fainali ikitokea Kundi A kwa kukusanya pointi sita na mabao matano baada ya mechi yao ya awali kuitoa nishai Yanga kwa mabao 2-1.
Katika mechi huo wa kwanaa Olunga anayewindwa na Simba, ingawa ni ngumu kumpata kwani ana mkataba wa miaka miwili, alifunga bao moja.
Kwa kufunga mabao hayo mawili jana, imemfanya kuongoza orodha ya wafungaji wa michuano hiyo akiwa na magoli matatu akimzidi kete Sallah Bilal wa Al Khartoum ambaye alikuwa akiongoza kwa mabao mawili baada ya mchana wa leo kuingoza timu yake kuilaza Telecom kwa mabao 5-0.
Mara baada ya mechi yake ya Yanga, Olunga alinukuliwa akisema kuwa amekuja Tanzania akiwa na nia moja ya kuwa Mfungaji Bora wa michuano hiyo, kitu kinachoonyesha ni kweli baada ya kufanikiwa kufunga mabao hayo mawili.
Kabla ya Olonga kufunga mabao hayo, Meddie Kagere mkali mwingine wa Gor Mahia aliifungia timu hiyo bao la mapema akimalizia pande la Olunga kabla ya KMKM kusawazisha na kwenda mapumziki timu zikiwa sare ya 1-1 mpaka kwenye dakika ya 65 Olunga alipoanza kufanya yake na kuwazamisha Wazanzibar.










Meneja
wa Manchester United Louis van Gaal Leo huko Old Trafford Jijini
Manchester alimtambulisha rasmi Mchezaji mpya Memphis Depay mbele ya
Wanahabari katika Mkutano maalum na pia kuthibitisha Mchezaji wa
Kimataifa wa Italy Matteo Darmian anaelekea England kukamilisha Uhamisho
wake kutoka Torino.
Nae Memphis Depay, mwenye Miaka 21 na
alienunuliwa Mwezi uliopita kutoka PSV Eindhoven ya Holland Klabu
aliyoisaidia kuwa Mabingwa Msimu uliopita huku yeye akiwa ndie Mfungaji
Bora wa Ligi, alisisitiza amejiunga na Manchester United ili kutwaa
Vikombe vyote vinavyowezekana na yeye atajituma hadi mwisho. 
KIUNGO wa kimataifa wa Uturuki, Arda Turan amekamilisha usajili wake katika klabu ya Barcelona baada ya kutia saini katika mkataba wa miaka mitano leo.
BAADA ya kuelekea kumpoteza mshambuliaji wake matata, Robin van Persie, klabu ya Manchester United imepanga kutoa kitika cha pauni Milioni 60 ili kumnasa mshambuliaji wa Kijerumani Thomas Muller.
