STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 16, 2013

TFF yashitakiwa mahakamani Mwanza



Na Faustine Feliciane
ALIYEKUWA mgombea wa nafasi mbili za Rais na mjumbe wa Kamati ya utendaji katika uchaguzi wa Shirikisho la soka (TFF) uliopangwa kufanyika Jumapili ijayo jijini Dar es Salaam, Richard Rukambula amefungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Mwanza kuzuia uchaguzi huo akishinikiza kurejeshwa kwenye mchakato.
Rukambula amefungua kesi hiyo itakayosikilizwa keshokutwa katika Mahakamu Kuu kanda ya Mwanza kupinga mchakato wa kumuengua kwenye uchaguzi huo kwa madai kuwa hakutendewa haki katika kuengeliwa kwake kwenye mchakato huo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana kutokea Mwanza, Rukambula alisema kuwa amefika hatua ya kusimamisha uchaguzi huo wa TFF ili suala lake lijadiliwe na haki itendeke kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
Wakati Rukambula akifikia hatua hiyo, Katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema shirikisho halijapata taarifa hizo lakini akasema pindi watakapoitwa mahakamani, vyombo husika ndani ya TFF vitakaa na kufanya maamuzi.
Rukambula amefungua kesi hiyo akisistiza hakutendewa haki katika kumuengua kwenye mchakato wa uchaguzi huo kwa maelezo kuwa aliomba nafasi mbili badala ya moja tu, kama inavyotakiwa.
"Tayari hili jambo limeshafika Mahakama Kuu kanda ya Mwanza na kesi imeshapangiwa jaji atakayesikiliza suala hili ," alisema Rukambula,
Aidha, alisema jalada la kesi hiyo lipo kwa Jaji Muruma.
"Leo hii (jana) nimemtuma mtu na anakuja huko Dar es Salaam na ndege ya jioni ili kuleta barua kwa TFF ya kuitwa Mahakamani kusikiliza kesi hiyo," alisema Rukambula.
Aidha, alisema ameiomba Mahakamu Kuu kuisikiliza kwa haraka kesi hiyo ili imalizike kabla ya siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa TFF; ili ikiwezekana arudishwe kwenye mchakato huo wa uchaguzi.
Aidha, alisisitiza kuwa maombi aliyoyapeleka mahakamani hapo ni ya kusimamisha uchaguzi huo ili mchakato wa kusaili wagombea urudiwe tena.
Rukambula anasema kuwa kamati ya uchaguzi ya TFF ilimuengua kwa madai kuwa aliomba kugombea nafasi mbili tofauti kwenye uchaguzi huo kitu ambacho ni kinyume na kanuni za uchaguzi wa TFF.
"Mimi sikuomba kugombea hizo nafasi kwa kufuata kanuni hizo wanazozisema bali nilifuata tangazo lao la uchaguzi walilolitoa ambalo halikuelezea kikomo cha kuwania nafasi kwenye uchaguzi huo," alisema Rukambula.
Aidha, alisema kuwa kama ni kosa kugombea nafasi mbili ni kwa nini TFF walikubali malipo yake ambapo alilipia fomu ya kuwania Urais na ile ya Ujumbe na kupewa stakabadhi zilizofuatana?

 CHANZO:NIPASHE JUMAMOSI

OMARY RAMADHANI ATWAA UBINGWA WA TAIFA WA PST




Bondia Omar Ramadhani akishangilia ushindi baada ya kumpiga Deo Njiku kwa point jana na kutawazwa kuwa bingwa wa taifa PST



Mabondia wakisubili matokeo ya mchezo



Mabondia Deo Njiku (kushoto) na Omary Ramadhani wakionyeshana umwamba juzi




Deo Njiku akimtupia konde Omary Ramadhani alioyeinama kulikwepa katika pambano lao la juzi



BONDIA Omary Ramadhani wa Dar es Salaam juzi alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Taifa wa PST baada ya kumshinda kwa pointi mpinzani wake, Deo Njiku katikia pambano kali lililochezwa klwenye ukumbi wa Friends Corners, Manzese Dar es Salaam.
Pambano hilo lililokuwa la uzani wa Light, liliishia hata hivyo kwa rabsha iliyofanywa na baadhi ya mashabiki wa ngumi wanaodaiwa ni wa mmoja wa mabondia hao waliokuwa wakilazimisha bondia wao atangazwe mshindi.
Mwamuzi wa pambano hilo alimtangaza Omar kubwa mshindi na kukabidhiwa mkanda wake wa ubingwa huo wa PST, huku Njiku akiiambia MICHARAZO kwamba matokeo hayo hayakumridhisha kwa kuhisi ni kama ya kupanga kwani anaamini alimzidi mpinzani wake.
"Japo mwenzangu ametawazwa bingwa, lakini ukweli sikubaliani na matokeo hayo naona kama yalipangwa na kuna mambo ambayo yalifanyika ukumbi sikuridhika nayo, hii ndiyo inayofanya ngumi zisiendelee," alisema Njiku ambaye tayari yupo mkoani Morogoro yalipo maskani yake.
Katika pambano hilo ambalo mabondia wote walionyesha ujuzi wa kutupiana makonde na kukwepana, kulikuwa pia na mapambano mengine ya utangulizi ambayo yaliwapa burudani mashabiki waliofika ukumbini hapo.

Baadhi ya michezo hiyo ya utangulizi ni lile la Godfrey Silva aliyemshinda kwa pointi Adam Yahya, Ramadhani Kumbele aliyempiga kwa pointi Shaabani Kilumbelumbe, huku Sadik Momba alifanikiwa kumpiga kwa pointi bondia Idd Mnyeke katika pambano lililovutia wengi.

   
Dkt, Milhael Arraham kushoto akimpima Afya Iddy Mnyeke kabla ya mpambano wake na Sadiki Momba juzi


Bondia Cosmas Kibuga kulia akimshambulia kwa makonde Makali mawe wakati wa mchezo wao uliofanyika juzi


Mashabiki na wapenzi wa mchezo wa masumbwi kutoka kambi ya Ilala akifatilia mpambao huo


Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Idd Mnyeke wakati wa mpambano wao uliofanyika juzi. Momba alishinda kwa point.


Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Idd Mnyeke wakati wa mpambano wao uliofanyika juzi.


Bondia Ramadhani Kumbele kushoto akioneshana kazi na Shabani Kilumbelumbe wakati wa mpambano wao uliofanyika juzi na Kumbele alishinda kwa point.


Mashabiki wa bondia toka kambi ya ilala Idd Mnyeke wakiwa katika picha ya pamoja na bondia wao


Bondia Adam Yahya (kushoto) akipambana na Godfrey Slva wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Taifa unaotambuliwa na PST. Silva alishinda kwa Point.


Bondia Ibrahimu Class ' Kking Class Mawe' akifatilia mpambano wa masumbwi uliokuwa ukifanyika  Dar es salaam jana pembeni yake ni mke wa kocha maarufu wa ngumi, Super D,  Bi. Asha Kamnyanga 'Mama Ikota'.


Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' akimkabidhi bondia Godfrey Silva vifaa vya mchezo wa masumbwi ikiwemo fulana, vikingia kinywa na DVD kwa ajili ya mafunzo ya mchezo huo.


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila  'Super D' kushoto akipiga picha ya pamoja na Godfrey Silva baada ya kocha huyo kumzawadia vifaa mbalimbali vya michezo.