STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 23, 2013

YANGA, AZAM NI VITA TUPU LEO TAIFA


KLABU zilizopo kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga na Azam leo zinatarajiwa kukutana katika pambano ambalo ni sawa na 'vita' katika mfululizo wa ligi hiyo.
Timu hizo zitakwaruzana kwenye mechi itakayochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku kila mmoja ikiwania ushindi ili kujihakikisha kukalia kiti cha uongozi kwa raha.
Yanga ndiyo inayoongoza msimamo wa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, ikilingana kwa pointi 36 na wapinzani wao Azam waliotangulia mbele kwa mchezo mmoja zaidi.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na ukweli kuwa timu zote zimeonyesha viwango vya juu kwenye michezo ya ligi kuu na zote zimekuwa zikifanya vizuri kwenye michezo hiyo.
Ubora wa kila kikosi ni mzuri kiasi kikubwa kwamba umetia hofu kila kocha wa timu hizo.
Akizungumza jana kocha Ernest Brandts wa Yanga alisema mchezo wa leo utakuwa mgumu kwao hasa kutokana na uwezo wa Azam walioonyesha kwenye michezo ya ligi kuu mzunguko huu wa pili.
Aidha alisema timu hiyo ya wauza vyakula ina morali ya juu baada ya kushinda mchezo wake wa Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika dhidi ya Al Nasri Juba ya Sudan Kusini.
"Mchezo hautakuwa rahisi... kwangu nategemea mchezo mgumu na wenye upinzani kwa sababu naamini timu zote zipo kwenye kiwango cha juu kwa sasa," alisema Brandts.
Aidha, alisema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na amepata nafasi ya kuiangalia Azam kwenye baadhi ya mechi zake hivyo anjua nini cha kufanya hili kujiwekea mazingira ya ushindi.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Azam ambayo imeshinda mechi zake zote nne za duru la pili lililoanza mwezi uliopita, ilifungwa kwa magoli 2-0 na Yanga kwenye uwanja huo wa Taifa.
Kocha wa Azam, Stewart Hall, amesema Yanga ni timu nzuri lakini wapo tayari kukabiliana nayo.
"Wana wachezaji wazuri na wanacheza kitimu lakini ukiangalia hata sisi (Azam) tuna wachezaji wazuri na timu imekuwa kifanya vizuri hivyo hakuna cha kutuogopesha," alisema Hall.
Hata hivyo, Azam inaweza kuwa kwenye wakati mgumu hasa kutokana na safu yake ya ulinzi kutokuwa kwenye kiwango cha juu hasa baada ya kuwasimamisha Aggrey Moris, Said Moradi na Erasto Nyoni waliokuwa wakiunda ukuta wa timu hiyo.
Lakini Azam kama ilivyo Yanga inajivunia safu kali ya ushambuliaji inayoongozwa na Kipre Tchetche ambaye amefunga magoli 10 kwenye ligi huku Yanga ikimtegemea Jerry Tegete mwenye magoli manne katika mechi tatu za ligi zilizopita.

Mtambo wa Gongo amtambia Kaseba



Bondia Maneno Osward akijifua kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa dhidi ya Japhert Kaseba March 2 katika ukumbi wa DDC Madomeni Kondoa Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' akifanya mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa dhidi ya Japhert Kaseba March 2 katika ukumbi wa DDC Madomeni Kondoa Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Maneno Osward kushoto na Japhert Kaseba walipokutana kwa ajili ya kuzungumzia mpambano wao utakaofanyika March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Maneno Osward ametamba kumchakaza mpinzani wake Japhert Kaseba kunako raundi za awali akizungumza na mwandishi wa habari hizi maneno maarufu kwa jina la Mtambo wa Gongo amesema yeye yupo fiti na anasubili hiyo March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni kondoa apate kumshikisha adabu 

Kaseba ni bondia mchanga sana kwangu nilimkaribisha katika masumbwi na sasa nitamstafisha masumbwi mimi mwenyewe kwa kipigo nitakacho mpa na atajua kwa nini nimepewa jina la mtambo wa Gongo

Katika mpambano huo kutakuwa na mpambano wa uzito wa juu kati ya Josefu Marwa na Alphonce Mchumiatumbo mpambano unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa ngumi za uzito wa juu nchini 

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.

--