STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, June 17, 2013

Langa Kileo kuzikwa leo, wengi wamlilia

Langa Kileo enzi za uhai wake
WAKATI mwili wa msanii wa kizazi kipya, Langa Kileo, aliyefariki Juni 13 ukitarajiwa kuagwa na kuzikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam, wasanii wenzake na watu mbalimbali maarufu wametoa salamu zao za pole wakionyesha kuguswa na vifo mfululizo vya wasanii nchini.
Baadhi ya wasanii na mastaa hao kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii wamesema kifo cha Langa ni kama kutoneshwa kidonda cha msiba wa Albeert Mangweha aliyefariki Mei 28 nchini Afrika Kusini na kuzikwa Juni 6 mjini Morogoro.
Wasanii kama Hammer Q, Nikki Mbishi, Joh Makini ambaye naye alikuwa akisumbuliwa na malaria, Fina Mango, Teddy Kalonga, MwanaFA wamelezea kusikitishwa na kifo cha Langa na kumtakia mapumziko mema.
Teddy Kalonga aliandika katika ukurasa wake wa facebook akihoji inakuwaje watu wengi wanakufa wakiwa vijana wadogo katika zama hizi, huku Joh Makini akiweka bayana kwamba hatatoa kazi yake yoyote mpya ili awaomboleze wasanii wenzake waliotangulia mbele ya haki.
Fina Mango yeye alitoa pole kwa baba na mama Langa Kileo na kuwataka kuwa na uvumilivu na subira katika kipindi hiki cha msiba wa mtoto hukuywao aliyemtakia safari njema huko aendako.
Langa Kileo alifariki jioni ya Alhamisi iliyopita baada ya kuugua ghafla na kukimbizwa Muhimbili na anatarajiwa kuagwa leo saa 7 kabla ya kuzikwa baadaye kwenye makaburi ya Kinondoni, huku msiba wa Ngwair na muigizaji Taji Khamis 'Kashi' ukiwa bado haijasahaulika baada ya kufululizana.

CHADEMA WATOA TAMKO JUU YA MLIPUKO WA BOMU LA ARUSHA

SAM_2023Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambae pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh Freeman Mbowe akitoa tamko la chama chake jioni ya leo katika hoteli ya Kibo Palace ya Jijini Arusha kufuatia tukio la kushambuliwa kwa mkutano wa Chadema jana kufunga kampeni za udiwani kwa Kata nne za Arusha Mjini kwa bomu la kutupa kwa mkono, risasi za moto na mabomu ya machozi, tukio lililopelekea vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.
SAM_2026Timu ya waandishi wa habari waliohudhuria kikao hicho cha kutoa tamko la chama.
SAM_2027

Tamko la Chadema Mauaji ya Bomu Mkutano wa Arusha: Mbowe asema tukio ni la kisiasa na lilipangwa makusudi; adai hata wakimuua yeye au Lema Chadema bado itaendelea kuwepo

Sunday, June 16, 2013

CCM, CHADEMA VITA TUPU IRINGA, MORO

MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wilayani Kilolo, Lunyiliko Nyaulingo amelazwa katika Hospitali ya mkoa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mgololo amelazwa Hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wanaodaiwa ni wanachama wa CCM katika kampeni za mwisho za kuwania nafasi ya udiwani.

Sambamba na hiyo Katibu wa CCM kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo, Wilhad Ngogo (40) na Yohana Mchafu anayedaiwa kuwa ni mwanachama wa CCM wanashikiliwa na Polisi kwa kuhusika na matukio hayo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema watu hao walikamatwa jana kufuatia 
vurugu zilizojitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya mwisho katika wilaya hizo mbili.

Alisema kufuatia mzozo huo wanachama wa CHADEMA walizuia barabara ya Iringa-Mbeya kwa kuweka magogo ili kuzuia magari kupita na kuwa Polisi wanamtafuta Rabart Sam maarufu kwa jina la Kideri kwa kuongoza vurugu hizo.

Kamanda Mungi alisema wanafanya uchunguzi wa kina juu ya matukio hayo na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha alitoa wito kwa viongozi wote wa vyama vya siasa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ili kuepusha vurugu ambazo zinaweza kutokea.

Leo Uchaguzi wa udiwani katika kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo na Mbalamaziwa wilayani Mufindi ulifanyika ambapo Zuberi Nyomolelo (CCM) na Ezekiel Mlyuka (CHADEME) walipambana kwa kata ya Mbalamaziwa na kwa upande wa Ng’ang’ange Kilolo Nafred Chahe (CHADEMA) na Namgalesi Msuva (CCM) walipambana.

Tukio hilo limejiri wakati huko Morogoro nako inaelezwa wanaodaiwa vijana walinzi wa CCM kuwakata mapanga viongozi wa CHADEMA, huku watanzania wakiendelea kuomboleza tukio la mlipuko wa bomu jijini Arusha lililopoteza uhai wa watu wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Katibu  Mwenezi wa tawi la Minepa, Jimbo la Ulanga Magharibi, Severin Matanila aliyekaa aliyejeruhiwa katika tukio la Morogoro, huku viongozi wenzake, Mwenyekiti wa Jimbo, Kibam Ally Mohammed na Katibu wake, Lucas Lihambalimo (aliyeipa kamera mgongo) wakiwa pembeni yake 
via Mjengwa