STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 30, 2013

Binti aoza mkono, kisa baiskeli


Janeth Nicholaus (25)mkazi wa Rwanzari Manispaa ya Tabora akionesha mkono wake wa kulia ukiwa tayari umeanza kuoza baada ya kupata ajali ya baiskeli maarufu daladala wakati akitokea nyumbani kwenda Soko kuu la Tabora mjini ajali ambayo ilitokea kwenye makutano ya barabara ya NBC. 

Huu ndio mkono wenyewe unavyoendelea kuharibika baada ya kupita hospitali kadhaa hapa Tabora mjini na kushindikana kupona lakini sasa aliamua kufika kwenye huduma ya Maombezi  Kanisa la AGAPE MIRACLE CENTER Mwanza road Tabora manispaa kwa Mchungaji Mbagata. 

NA KAPIPIJ

Vipaji vya soka mkoani Tanga hivi hapa!

Mchezaji wa timu ya Watukutu kulia Idrisa Bakari akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya Sepras ya jijini Tanga wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika katika viwanja vya walewale Makolola jijini Tanga.
Mchezaji wa jimu ya Sepras Hassani Abdallah akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Watukutu wakati wa mchezo wao wa kirafiki.
Timu ya Sepras
Nyota wa baadaye

Wapenzi wadondoka na kufa wakifanya mapenzi dirishani

Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China.

Wawili hao wanasemekana kudondoka kutoka kwenye dirisha la jengo moja la makazi kwenye jiji la Wuhan nchini humo pale dirisha hilo walilokuwa wameegemea kufunguka.


Mashuhuda walivieleza vyombo vya habari vya China kwamba wapenzi hao walikumbatiana wakati wakianguka kwenye njia ya waenda kwa miguu nje.

Kwa mujibu wa The Sun, chanzo kimoja cha habari kilisema: "Huku wawili hao wakiwa wameshikamana vilivyo, walianguka nje ya jengo hilo."

Picha za kuogofya zimefichuliwa kwenye tovuti za nchini humo zikionesha wapenzi hao wakiwa wamefunikwa kwa mashuka na polisi.

Damu ilitapakaa kwenye njia ya waenda kwa miguu karibu na wapelelezi wanaonekana wakichunguza eneo la tukio.


Miili ya wapenzi hao ilipigwa picha karibu na baiskeli ambayo ilikuwa imelazwa chini, lakini hakukuwa na ripoti zozote kwamba yeyote chini alikuwa amejeruhiwa katika ajali hiyo.

Ripoti zinasema kwamba madirisha hayo kwenye jengo hilo la makazi yalikuwa hayana ubora unaotakiwa.

Inafikiriwa kwamba mwanaume huyo na mwanamke wanawezekana walikuwa wakijaribu kujipooza kando ya dirisha hilo ndipo tukio hilo likatokea.

Haikufahamika ni umbali gani kutoka juu wawili hao walikuwa wakati wakianguka.
 

Wuhan ni jiji maarufu zaidi lililopo katikati ya China.
Ukiwa na historia ya miaka 3,500 ni moja kati ya miji mikongwe na iliyostaarabika katika China.


zero99

Saturday, June 29, 2013

Hivi ndivyo Golden Bush ilivyoizima Chuo Kikuu Veterani


Wachezaji wa Golden Bush na Chuo Kikuu wakiwania mpira hewani

Kudra Omar akizidhibitiwa na beki wa Chuo Kikuu Veterani

Mtanikoma leo

Kudra Omar 13, akitafuta mbinu za kumtoka Ernest





Nasema faulo, jipangeni pale:Refa akiwaelekeza wachezaji wa Chuo kujipanga ilia Golden Bush wapige faulo

Heka heka langoni mwa Chuo Kikuu veterani

Mchesaji wa Golden Bush akiwa chini baada ya kuumia
 
Salum Swedi 'Kussi' akionyesha kiwango uwanjani

Mshikemshike dimbani

Kipa Amani Simba akiwapanga mabeki wake wakati wa kupigwa faulo langoni mwake.

John Mwansasu na Wazir Mahadh 'Mandieta' wao walikuwa mashuhuda tu kwa leo

Hawa Madogo wanakaza niingie nini?

Kudra Omar na salum Athuman wakiwa kwenye mapumziko

Amani Simba, Onesmo Wazir 'Ticotico' na Salum Swedi 'Kussi' wakiwa kwenyue mapumziko

Hoi mapumziko hata kama tunaongoza 2-1

Kocha Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' akiwapa nasaha wachezaji wake wa Golden Bush


Mmecheza vyema, lakini mabao hawatoshi; kocha msaidizi, Herry Morris akiwapwa nasaha wachezaji wake
Mmekosaje bao pale nyie...enzi zangu yule kipa angekuwa analilia atolewe nje kuepuka kapu la mabao

Jamani jahazi linazama nyumbani inajuwake sasa?
Benchi la ufundi la Chuo Kikuu veterani hawaamini kinachowakuta




Wachezaji wa Golden Bush wanamchezea rafu mchezaji wa Chuo Kikuu

Aaaghhh! Shija Katina akiugulia maumivu

Utanijua kwa nini naitwa 'Mbududu'

Kwa nini wanaume ulala wamalizapo kusex?JAMBO hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu mzima kama kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao, pale wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.

Lakini utafiti uliofanywa hivi na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni katika kuepuka lawama hizo, kwamba, kumbe siyo hiyari yao, bali ni maumbile.

Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la kujamiiana. 


Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.

Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.

Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.

"Utafiti huu unatupa matokeo ya kile kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.” Gazeti la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae Serge Stoleru.

“Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.

Mwanasayansi huyo aliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala baada ya kumaliza tendo il hali wao wakitaka zaidi….

Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake kuwalaumu tena wanaume baada ya kumaliza tendo na kulala kwa sababu hivi sasa wameshajua sababu, watuwache tupumuwe……

Source: Jamii Forums

Golden Bush Veterani wainyuka Chuo Kikuu Veterani 2-1


Beki wa Chuo Kikuu veterani Ernest akimtoka Kudra Omar katika pambano lao la leo

Kudra Omar akichuana na beki wa Chuo Kikuu katika mechi yao ya leo
Beki wa Chuo Kikuu akihamisha mpira langoni mwake huku kipa wake Idd akimshuhudia

Heka heka langoni mwa Chuo Kikuu
Ernest akikokota mpira mbele ya Kudra Omar
Nasafisha! Beki wa Chuo kikuu akihamisha  mpira langoni mwake
Onesmo Wazir 'Ticotico' akionyesha kiwango dimbani

Kiungo Shija Katina (8) wa Chuo Kikuu akimtoka Salum Athuman 'Mbududu' wa Golden Bush
Viungo nyota wa zamani nchini Shija Katina (8) na Salum Athuman wakionyeshana kazi
Hupati kitu hapa 'Mbududu'
Shija Katina akimiliki mpira mbele ya Abuu Ntiro

Benchi la Chuo Kikuu likiwa haliamini kama wamelala nyumbani
Beki wa kushoto wa Chuo Kikuu, Ernest (16) akitafuta mbinu za kumtoka Omar Mgonja wa Golden Bush, huku Yahya Issa naye akimpigia mahesabu
MABAO mawili yaliyotumbukizwa wavuni na nyota wa zamani wa Yanga, Kudra Omar na Abuu Ntiro asubuhi ya leo yalitosha kabisa kuipa ushindi wa mabao 2-1 timu ya Golden Bush Veterani dhidi ya wapinzani wa jadi Chuo Kikuu Veterani katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa Chuo Kikuu.
Golden Bush waliochezesha kikosi tofauti na kile walichokitangaza awali, ilianza kutanguliwa kufungwa bao kupitia kwa Paul mshambuliaji aliyekuwa akiikosesha amani ngome wa Golden Bush iliyokuwa chini ya Salum Swedi 'Kussi', Yahya Issa, Shomari na Omar Mgonja na kipa Aman Simba.
Hata hivyo Golden Bush iliyokuwa ikiongozwa katika safu yake ya ushambuliaji na Kudra Omar, Abuu Ntiro, Onesmo Waziri 'Ticotico' wakiungwanishwa vyema katikati na Godfrey Bonny 'Ndanje' Salum Athuman 'Mbududu'walirudisha bao hilo kupitia kwa Kudra Omar.
Dakika moja kabla ya mapumziko, Golden Bush waliongeza bao la pili lililofungwa na Abuu Ntiro baada ya kutokea pia nikupige klatika lango la Chuo Kikuu lililokuwa chini ya kipa Idd aliyejitahidi kuokoa mabao licha ya kwamba amezoeleka kucheza mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ya wachezaji na kuongeza kasi ya mchezo, na hasa Chuo Kikuu Veterani ambayo ilikuwa ikiunganishwa vyema na Shija Katina aliyeng'ara dimba la kati ambayo ilicharuka kutaka kusawazisha bao lakini kikwazo kikawa ukuta wa wapinzani na hasa kipa Amani.
Mpaka filimbi ya mwisho ya mwamuzi aliyelichezesha vyema pambano hilo, Mwenyekiti wa Chuo maarufu kama 'Obama', ilipolia Golden Bush walikuwa wababe mbele ya wapinzani wao waliokuwa uwanja wa nyumbani kwa kuwalaza mabao 2-1.