STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 30, 2013

SHEREHE YA WAFANYAKAZI WA IPP MEDIA ZILIZOFANA JANA


Watu walikuwa wkaitabasamu muda wote

Umakini nao ulikuwa muhimu ili kufuatilia matukio ukumbini

eeh wacha nicheke mwanakwetu!

Mpaka kieleweke hapa

Mtaalam Sultan akitabasamu kwa mbali


We pale unaelewa wanafanya nini? Ni kama wanaulizana

Kwa raha zetu

Kula bata kwa kwenda mbele

Ooh anataka kuharibu yule au Kiwewe unasemaje?

Mmeremeto kwa sana

Hayaa unajua sikujipanga kwa picha bana!


Mmoja wa waliong'ara kwa kunyakua tuzo, Angel Navuri

Raha ya Dunia
Kazi na dawa jamani mwili haujengwi kwa matofali

Mwili hujengwa kwa msosi au vipi!

Msosi kwanza

Sivunji mbavu hapa mpaka tumbo lienee

Kumbukumbu muhimu

Hatufukii twala kawaida






























Mamaaaa!









MAITI AZIKWA MARA MBILI KWIMBA MKOANI MWANZA.


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mwili wa kijana umezikwa mara mbili, baada ya maziko ya kwanza kufanywa na wanakijiji cha Mwalubungwe Kata ya Hungumalwa Kwimba, Mwanza, baada ya kumuua wakidhani jambazi na kumzika bila nguo wala sanda.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, baba mzazi wa kijana huyo, Seni Kamera alisema mwanawe Valence Abel (23), mkazi wa Zunzuli, Shinyanga, alikuwa akiishi Kahama kwa mganga wa kienyeji, akipata matibabu ya upungufu wa nguvu za kiume.

Alisema mwanawe huyo aliishi kwa mgan
ga huyo kwa miaka miwili bila kurudi nyumbani. 

Alidai wiki mbili zilizopita, aliamua kuondoka kwa mganga huyo kwa miguu akiwa amefuga ‘rasta’ na kuvaa kaniki na ngozi, masharti ambayo alipewa na mganga wake ili tatizo lake liweze kumalizika.

Alisema akiwa njiani kurudi nyumbani, alifika katika kijiji cha Mwalubungwe, na kwenda nyumba ya mkazi wa kijiji hicho kuomba chakula kutokana na njaa.

“Alipofika katika nyumba hiyo alikuta watoto wanacheza nje.Kwa mwonekano aliokuwa nao, walimpiga kwa mawe na kumwita mwizi, kisha mzazi mmoja akapigana naye huku akipiga kelele, watu walifika na kumshambulia na hatimaye alipoteza maisha na kumzika bila nguo wala sanda,“ alisema Kamera.

Alisema taarifa za kifo cha mwanawe, alizipata kwa mtu aliyemwambia kuna mtu ameuawa ambaye alijitambulisha kwa jina la Kamera.

Alifuatilia na kufukua kaburi hilo na kukuta ni mwanawe. Alichukua maiti na kumzika tena.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alipohojiwa kuhusu tukio hilo, alisema hana taarifa. Lakini, aliahidi kufuatilia ili kufahamu undani wake.
CHANZO HABARILEO.

Sumaye awapiga kijembe wapenda rushwa


Waziri Mkuu wa zamani, Mhe. Fredrick Sumaye

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ameibuka tena na kusema, wanaokerwa na karipio lake kuhusu rushwa, wanapaswa kuachana na vitendo hivyo viovu.
Hivi karibuni, Sumaye, alitoa karipio kwa viongozi wa dini hususani ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), akionya kuhusu kasi ya wanasiasa kutumika katika harambee zake.
Sumaye, alikaririwa akisema miongoni mwa wanasiasa hao, wanatumia mwanya huo kama njia ya kuungwa mkono watakapotangaza kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Ingawa hakuwataja wanasiasa hao kwa majini, kauli yake ilitafsiriwa kumgusa Waziri Mkuu ‘aliyemrithi’ na baadaye kujiuzulu, Edward Lowassa.
Lowassa ameshiriki harambee mbalimbali nchini, hali inayoelezwa na baadhi ya wachunguzi wa mambo ya siasa kuwa ina lengo la ‘kujisafishia’ njia kuelekea urais wa 2015.
Lakini Lowassa amekanusha kushiriki harambee hizo kwa nia ya kutafuta urais, badala yake akasisitiza kwamba ana karama ya ushawishi inayomfanya afanikishe shughuli hizo kwa kupata fedha nyingi.
Jana, Sumaye alizungumza na vijana wa klabu za Jogging za Ukwamani na Islamic katika uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam jana.
Alisema kama mtu anaumizwa na karipio lake dhidi ya vitendo vinavyoashiria rushwa, anapaswa kuachana navyo na si kumjibu kwa kejeli.
Sumaye alisema ushiriki wake katika vita dhidi ya vitendo viovu kama rushwa, umeanza muda mrefu na kwamba hata karipio lake kwa wanaousaka uongozi kwa njia zisizo sahihi ni sehemu ya kuisimamia imani na dhamira yake.
Alisema, “kama kuna mtu anayeumizwa kwa kauli zangu ninapokaripia uovu, nikipinga rushwa basi watoaji na walaji rushwa waache kujihusisha na vitendo hivyo, na kama hawataki kusemwa basi wapasuke.”
Sumaye alisema si rahisi akaacha kukemea vitendo viovu hasa vinavyofanywa na viongozi kwa sababu, ukimya ni sehemu ya kishawishi kwa waovu kuendeleza vitendo viovu.
Akimnukuu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliposema, serikali ya wala rushwa haiwezi kuleta maendeleo kwa wananchi wake.
Sumaye rushwa ikiachwa ishamiri, itakuwa vigumu kujenga nchi yenye usawa, hivyo kuifanya nchi kuwa katika hatari ya kuangamia.
“Hivi sasa imebaki miaka miwili ya kuingia katika Uchaguzi Mkuu, hivyo tutaanza kushuhudia namna kanga, kofia, fedha na vitu vingine vitakavyotembezwa kwa ajili ya kutafuta uongozi. Tusipolisema sasa, tutaangamia,” alisema.
Alisema wananchi wanapaswa kuwa makini na viongozi wanaotumia ushawishi wa fedha na rushwa, kwani hawafai kuongoza.
Alisema viongozi wa aina hiyo wana kundi la watu nyuma yao, wanaowafadhili hivyo pindi watakapopata uongozi, watalazimika kuwatumikia waliomo katika ufadhili huo.
Alipinga dhana kuwa vijana ni kama bomu linalongoja kulipuka, badala yake ameitaka serikali kuhakikisha wanapata fursa ili wazitumie kuliko kuwaita kwa majina hatarishi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Azam Academy yainyuka Ashanti Utd

Azam Academy jana ilicheza na timu ya Ligi kuu ya Ashanti United kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume Ilala na kushinda kwa bao moja bila goli likifungwa na Mshambuliaji wa pembeni toka shinyanga Mange 

Vijana wa Azam Academy wanaonolewa na kocha Vivek Nagul akisaidiwa na Iddi Cheche chini ya meneja Philip Alando walicheza kandanda safi na kuwapoteza kabisa vijana wa Ashani United wanaocheza ligi kuu Tanzania.

Mechi hii ya kirafiki ni ya tatu ndani ya siku nne ambapo siku ya jumatano Azam Academy ilishuka kwenye uwanja wake wa nyumbani na kukwaana na timu ya Transit Camp inayoshiriki ligi daraja la kwanza na kuiangushia kipigo cha 3-1, katika mchezo huo ambao uliacha gumzo kutokana na Azam Academy kutawala mchezo huo wakipiga pasi wanavyotaka.

Baada ya mechi hiyo viongozi wa Transit Camp walikwenda kwa uongozi wa Azam FC na kuwapongeza na kusema kama timu hii ingekuwa inashiriki ligi daraja la kwanza hakika ingeweza kupanda ligi kuu bila matatizo yoyote.

Wachezaji wanaotia fora kwenye kikosi hicho ni Kaijage, Rey, Dismas, Kevin Friday, Mkomola, Mgaya, Mange, Adam Juma, Jamir Brison na Adam Gambo.

Jumamosi Asubuhi licha ya kucheza vizuri na kutawala sehemu kubwa ya mchezo lakini walijikuta wakipokea kipigo cha goli moja bila bao likifungwa na Brian Umony ambaye alitumia vizuri mchezo wa mtego wa counter attack
TIMU ya vijana ya Azam, Azam Academy jana iliinyuka timu ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Ashanti United kwa bao 1-0 katika pambano la kujipima nguvu lililochezwa uwanja wa Karume Ilala.
Vijana hao walipata ushindi huo kupitia bao tamu lililofungwa na mshambulia wao kutoka mkoani Shinyanga aitwaye Mange.
Azam Academy inayonolewa na kocha Vivek Nagul akisaidiwa na Iddi Cheche chini ya umeneja wa Philip Alando waliwafunika kabisa Ashanti kwa soka murua walililoionyesha.
Hiyo ilikuwa mechi ya tatu kwa timu hiyo ya Azam Academy ndani ya siku nne ya awali kuumana na Transit Camp inayocheza Ligi Daraja la Kwanza na kuwakung'uta mabao 3-1 kabla ya kulala bao 1-0 toka kwa kaka zao Azam Fc katika mechi iliyofuata.