STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 2, 2013

Timu ya Kikapu ya UDSM ikijifua









BAADHI ya wachezaji wa timu ya kikapu ya Chuo Kikuu UDSM wakijifua kwa mazoezi kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Chuo Kikuu Mlimani-Dar es Salaam.

Njemba yaumbuka Sabasaba kwa kukwapua simu

KIBAKA ALIEIBA SIMU KATIKA BANDA LA VETA SIMU YA STAFFUWA VETA LEO
KIBAKA AMBAYE ALISHIRIKIANANA MWENZAKE KUIBA SIMULEO
KIBAKA ALIEIBA SIMU NAKUFANIKIWA KUKIMBIA LAKINI ALIBAMBWA LEO
AFISA WA NSSF AKITOA KITABUWATU MBALIMBALI WALIOTEMBELEABANDA HILOLEO
WASANIIWAKUNDI LA TOTI WAKIPOKEA VITABU KUTOKA KWA AFISA WA NSSF LEO
AKIONYESA BAADHI YUA VIKOMBE WALIVYOSHINDA
AFISA WA NSSF WAKIWAFAHAMISHA WATU MBALIMBALI WALIOFIKAKWENYE BANDA HILO LEO
KIKUNDI CHA SACCOS WALIOPATA KUPITIA NSSF
KIKUNDI CHA SACCOSICHA NSSF AMBAOWAMEFANIKIWA KUPAT MKOPO KUPITIA SACOSI WAKIWA NA DUKA LAO
KIKUNDI CHA TOTI
THEOPITA MICHAEL KUTOKA VETA  HOTEL NA UTALII KUTOKANJIRO ARUSHA AKIMUONYESHA MKURUGENZIMKUU WA VETA ZEBADISH MOSH KULIA CHUPA YA WINE INAYOTENGENEZWA NJIRO ARUSHA LEO
MKURUGENZI MKUU WA VETA ZEBADISH MOSH KUSHOTOAKIANGALI BAADHI NGUA ZINAZOTENGENEZWA PUGUKATIKA KIWANDA CHA TMBE KULIA NI ANGELA SAMUEL

Wanariadhaa Wa Dar wakijifua tayari kwa mashindano







Baadhi ya wanariadhaa wa jijini Dar es Salaam wakijifua kwenye viwanja vya Chuo Kikuu kujiandaa na mashindano mbalimbali.

Ubungo ipo hivi Obama akisubiriwa





Wakora wamkata binti mikono, kisa kinasikitisha



Picha hii haihusiani na habari hii
GENGE moja nchini India limekata mkono wa binti mmoja mwenye miaka minane kwa kutumia fyekeo huku familia yake ikijaribu kuhakikisha kuachiwa kwa kaka yake aliyetekwa nyara.
Uzma Ara alisafiri kwenda Patna, mjini Bihar, mashariki mwa India, akiwa na familia yake kwa lengo la kumkomboa mtoto huyo wa kiume mwenye miaka minne ambaye alikuwa amenyakuliwa kwenye mtaa mmoja karibu na nyumbani kwao katika wikaya ya Darbhanga.
Baba wa Uzma, Ainul Ansari anadai genge hilo lilimlenga binti huyo kutokana na kuwa shuhuda mkuu wa tukio hilo la utekwaji wa mtoto wake, Julfikar.
Vyombo vya habari vya India vimeripoti binti huyo yuko mahututi kwenye hospitali moja ya serikali mjini Patna baada ya kupoteza sehemu ya mkono wake wa kulia.
Familia hiyo imesema binti huyo alishambuliwa karibu na stesheni ya treni mjini humo Ijumaa wakati wakitafuta hoteli ya kukaa.
Ansari alisema kundi hilo liliwafuata hadi Patna ambako walikuwa wanatarajia kufungua mashitaka polisi.
Serikali ya Janata Dal inayoongozwa na Waziri Mkuu Nitish Kumar sasa imeamuru uchunguzi mpya wa shambulio hilo na mtoto wao wa kiume aliyepotea.
Mama wa Uzma, Nasreem Khatoon alimpinga moja kwa moja waziri mkuu huyo kwenye mkutano wake wa kila wiki.
Familia hiyo inasema polisi wa eneo hilo wameendelea kumshikilia mtoto huyo aliyepoteza mkono wake kwenye ajali ya treni.
Ansari ambaye ni fundi cherehani, alisema amekuwa akilazimishwa kulilipa genge hilo Pauni za Uingereza 3,300 kwa miezi michache iliyopita, imeripotiwa.
Anasema kwamba polisi wamegoma kuchunguza pale familia hiyo ilipogoma kulipia zaidi, genge hilo lililomteka mtoto wao.
Wanasiasa wa upinzani sasa wameishutumu serikali ya mjini humo kwa kushindwa kuchunguza madai hayo moja kwa moja.
Msemaji wa chama cha Bharatiya Janata, Shahnawaz Hussain alinukuliwa na Shirika la habari la Gulf akisema kwamba waziri mkuu huyo amechangia 'kuanguka kabisa kwa sheria' mjini Bihar.

Julio kutupiwa virago Simba kama Kaseja


Julio kwenye kijitabu akiwa na makocha wenzake kwenye mazoezi ya Simba uwanja wa Kines hivi karibuni
KOCHA Msaidizi wa klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' yupo katika hati hati ya kutimuliwa ndani ya klabu hiyo ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa kipa tegemeo, Juma Kaseja kufungashiwa virago vyake Msimbazi.

Kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na gazeti la NIPASHE ni kwamba maamuzi ya kutimuliwa kwa Julio kunatokana na kumaliza mkataba wake wa muda mfupi na tayari maamuzi yameshapitishwa na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ili nafasi yake ichukuliwe na Seleman Matola.
 Mmoja wa vigogo wa Simba aliyenukuliwa na gazeti hilo alisema kuwa tayari maamuzi ya kuachana na Julio yameshatolewa na nafasi yake itachukuliwa na kiungo na nahodha wa zamani wa timu hiyo, Matola.
Kigogo huyo alisema vilevile kuwa katika kikao hicho, watajadili maandalizi na kupanga siku ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa mwaka wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

"Sasa presha imehamia kwa Julio ambaye hatma yake haijulikani ndani ya Simba, lakini kilichopo ni kama ilivyokuwa kwa Kaseja," alisema kigogo huyo.
Julio alipotafutwa kuelezea hatma yake, alisema yuko kwenye kelele na atafutwe baadaye ambapo hakupatikana tena kupitia simu yake ya mkononi.

Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, aliliambia gazeti hilo kuwa ni kweli kesho kamati ya utendaji itakutana lakini kubwa watakalojadili ni kupanga maandalizi ya wiki ya Simba.

Mtawala alisema kuwa kikao hicho kitabariki shughuli zote za kijamii zilizopangwa kufanyika na kumalizika kwa tukio la kutambulishwa kwa wachezaji wapya wa Simba katika siku ijulikanayo kama 'Simba Day'.

Alieleza pia zoezi la usajili wa wachezaji wapya limeenda kwa umakini na kwa zaidi ya asilimia 80 wamekamilisha mchakato huo.

Alisema kabla ya kuanza kwa msimu mpya, timu hiyo inatarajia kuweka kambi nje ya jiji la kucheza mechi za kirafiki zaidi ya tatu kwa ajili ya kuwaandaa na kuwaweka tayari kukabiliana na ushindani katika msimu ujao wa ligi.

Simba sasa inaendelea na mazoezi chini ya kocha wake mkuu, Abdallah Kibaden 'King' wakati Matola akiendelea kuisimamia timu ya vijana (Simba B).

Mfalme Mswati aitimka zake kwao Swaziland


Mfalme Mswati wa Swaziland akisindikizwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipoondoka kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam kurejea nyumbani baada ya kufungua maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerere Julai 1,2013.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na mfalme Mswati wa Swaziland ambaye aliondoka nchini baada ya kufungua maonyesho ya Kiataifa ya Biashara kwenye uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Arsenal yamnyakuwa kinda la kifaransa ni Yaya Sanogo

Yaya Sanogo
KLABU ya Arsenal imethibitisha katika tovuti yake kwamba mwanasoka kinda wa kimataifa wa Ufaransa, Yaya Sanogo amesaini Mkataba wa muda mrefu kwao. 
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amejiunga kwa ada ndogo tu baada ya kumaliza Mkataba wake klabu ya Daraja la Kwanza Ufaransa, Auxerre. 
Sanogo kwa sasa yupo na timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 20, katika Kombe la Dunia la U-20, akiwa amefunga mabao mawili kati ya matatu ya timu yake nchini Uturuki, na amefunga mabao tisa katika mechi 13 katika msimu alioandamwa na majeruhi Ufaransa.
Gonzalo Higuain na Wayne Rooney ni washambuliaji wengine walioripotiwa kutakiwa The Gunners msimu huu, lakini Wenger anavutiwa mno na uwezo wa Sanogo.
"Sanogo ni usajili mzuri wa kinda kwetu,"aliiambia Arsenal.com. "Ameonyesha uwezo wake siku za karibuni akiwa na Auxerre na poa kikosi cha vijana chini ya miaka 20 cha Ufaransa.
"Tunasonga mbele kwa Yaya kujiunga nasi na kuendeleza kukuza kiwango chake,"alisema Wenger.
Zoezi hilo lipo kwenye kukamilisha taratibu za kawaida za usajili na Sanogo atajiunga na wenzake baada ya mashindano ya Uturuki.

Hivi ndivyo Rais Obama alivyopokelewa Tanzania

RAIS OBAMA akiteremka kwenye Air Force One na mtoto wake pembeni mara baada ya kuwasili katika ardhi ya Tanzania wakati akitokea afrika ya Kusini jana mchana kwa ziara ya kikazi nchini.Barack Obama akipokewa na Wananchi wa  Tanzanian huku wanaband wakitumbuiza nyimbo mbalimbali kwenye uwanja wa Mwl.Julius Kambarage jijini Dar es Salaam jana mchana akitoka Africa kusini.


Rais Obama akipita kwenye kapeti jekundu huku akiwa na furaha na kucheza nyimbo za wabongo kwenye uwanja wa jijini Dar es salaam wa Mwl. Julius Kambarage mchana wa jana.

Karibu  Tanzania....karibu!!!

Ilikuwa ni patashika kwa wacheza ngoma hapa!!! Obama mpaka akaachia Tabasamu

Rais Obama akicheza nyimbo za hapa kwetu Bongo huku akiwa na furaha kwa mapokezi baada ya kukanyaga ardhi ya Tanzania jana.U.S. President Barack Obama participates in an official arrival ceremony at Julius Nyerere Airport in Dar es Salaam, Tanzania, July 1, 2013. REUTERS-Jason ReedU.S. President Barack Obama walks with Tanzanian President Jakaya Kikwete during an official arrival ceremony at Julius Nyerere Airport in Dar es Salaam July 1, 2013. REUTERS-Jason ReedObama na JK.U.S. President Barack Obama and first lady Michelle Obama receive flowers, as their daughter Sasha (2nd R) watches, during an official arrival ceremony at Julius Nyerere Airport in Dar es Salaam, Tanzania, July 1, 2013. REUTERS-Jason ReedKaribu Baba ! Karibu Tanzania!

Rais na First Lady Obama wakisalimia wananchi wa Tanzanian baada ya kupokewa na Rais Jakaya Kikwete na First Lady Salma
Ni furaha hapa baada ya Rais Obama kutua Bongo, hapa anaonekana na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete wakipokewa kwa ngoma Ni mimi jamani ...tupo pamoja !. Karibu jamani ....jaribu mzee!!! Tunakupenda!! Mapokezi haya!!! angalia mavazi!!  Rais Barack Obama wa Marekani (kushoto) akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari wa Tanzania na Kimataifa Ikulu Jijini Dar es Salaam jioni YA JANA ambapo mbali na kuzungumzia mstakabali wa ziara yake nchini Tanzania na Afrika pia amezungumzia masulala mbalimbali ya Kimataifa ukiwepo mgogoro na Vurugu zinazoendelea nchini Misri na Congo DRC.