STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 15, 2013

Kuziona Yanga na Azam Buku 7 tu

Na Boniface Wambura
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga na makamu bingwa Azam wanavaana keshokutwa (Jumamosi) kwenye mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa 2013/2014.

Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kivutio kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni ambapo mshindi atakabidhiwa ngao.

Iwapo dakika 90 za mechi hiyo hazitatoa mshindi, timu hizo zitatenganishwa kwa mikwaju ya penalti huku asilimia 10 ya mapato ya mechi hiyo yakienda kwa kituo cha kulelea watoto cha SOS.

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000. Watakaiongia viti vya VIP C watalipa sh. 15,000, viti vya VIP B ni sh. 20,000 wakati VIP A watalipa sh. 30,000.

News Alert; Sheikh Ponda aondolewa hospitali na kupelekwa Segerea?

HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda amehamishwa toka hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kupelekea gereza la Segerea.
Habari hizo zinasema askari Polisi wamefika hospitalini hapo na kuondoka na Sheikh Ponda ambaye jana alisomewa mashtaka akiwa kitandani.
Tunafuatilia kujua ukweli wa jambo hili sambamba na kujua kilichosababisha Sheikh huyo kukimbizwa huko wakati akiendelea kupata matibabu ya jehara alilolipata kwa kilichoelezwa kupigwa risasi na Polisi mjini Morogoro mwishoni mwa wiki wakai wa shamrashamra za sikukuu ya Eid el Fitry.

LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA SEPT 14


Na Boniface Wambura
MICHUANO ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu msimu huu (2013/2014) itaanza kutimua vumbi Septemba 14 mwaka huu.

Kila timu itakayoongoza kundi lake katika ligi itakayochezwa kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini) ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015.

Mechi za ufunguzi kwa kundi A zitakuwa kati ya Tessema vs Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam) wakati Septemba 15 mwaka huu ni Transit Camp vs Polisi Dar (Uwanja wa Mabatini, Pwani), Ndanda vs Friends Rangers (Uwanja wa Nangwanda, Mtwara) wakati Villa Squad vs African Lyon itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kundi B ni Burkina Faso vs Polisi Moro (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Mkamba Rangers vs Lipuli (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro), Majimaji vs Mlale JKT (Uwanja wa Majimaji, Songea) wakati Septemba 15 mwaka huu Kimondo SC vs Kurugenzi (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).

Mechi za ufunguzi kundi C ni Polisi Mara vs Polisi Dodoma (Uwanja wa Karume, Musoma), Kanembwa JKT vs Polisi Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma), Stand United vs Mwadui (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), na Pamba vs Toto Africans (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).

Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 26 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Machi 22 mwakani.

Wednesday, August 14, 2013

Serikali yaingilia kati mzozo wa Yanga na Azam Media

HATIMAYE mkutano ulioitishwa na serikali kupitia wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kusuluhisha mgogoro wa mkataba wa mauzo ya haki za matangazo ya Television uliowashirikisha kamati ya ligi kuu ya soka Tanzania bara, klabu ya Yanga na Azam Media umemalizika hivi punde huku maamuzi kadhaa yakifikiwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha mtandao huu, klabu ya Yanga ni kama imeibuka kidedea kwenye madai yake ya kupinga utaratibu mzima wa mkataba huo baina ya kamati ya ligi na Azam Media. 

Hii inakuja baada maamuzi ya mkutano huo kuamuru kwamba vipengele vya mkataba huo kupitiwa upya na klabu ya Yanga na Kamati ya Ligi na vile ambavyo vitaonekana kuwa na matatizo virekebishwe. 

Pia imeamuliwa kwamba Yanga SC itakaa kikao na Azam Media kuzungumzia mambo mbalimbali ambayo Yanga imeonekana kuwa na shaka nayo kuhusu Azam pamoja na maslahi ya Yanga kupitia dili hilo la ununuaji wa haki za matangazo ya TV ya mechi za ligi uliofanywa na Azam Media.  


Shafii Dauda

Ni Mauaji Kila Kona Mbeya


 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



WILAYA YA MBOZI – MAUAJI
MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA SAA 07:00 HRS UKO KIJIJI CHA NANSAMA KATA YA ISANSA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. SIJAONA S/O HAONGA MIAKA 45, MKULIMA, MNYIHA, MKAZI WA NANSAMA ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KUTUPWA KATIKA MTO MLOWO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI MGOGORO WA MASHAMBA KATI YA MAREHEMU NA SHABANI S/O MBWILI PAMOJA NA MAWAZO S/O MBWILI AMBAO WALITOROKA MARA BAADA YA TUKIO HILO.  MAREHEMU ALIVIZIWA WAKATI   AKIVUA SAMAKI NA PEMBENI YA MWILI WAKE KULIKUTWA NDOANO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  KUTOJICHULIA SHERIA MKONONI NA KUITATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA  MAZUNGUMZO  NA  YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.
WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI
MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA SAA 00:05 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANGA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.  MARIA D/O MARTIN, MIAKA 37, MNYAMWEZI, MKULIMA, MKAZI WA KANGA ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI KICHWANI NA KUKABWA SHINGONI NA MPENZI WAKE AITWAE LAMECK S/O MSANGAWALE, MIAKA 35, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KANGA.  CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MTUHUMIWA KUMKUTA MAREHEMU AKIWA NA MWANAUME MWINGINE. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUYATATUA MATATIZO YAO YA KIJAMII KWA NJIA YA MEZA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA. PIA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO MAENEO YA UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA IBRAHIMU S/O MATSON ,MIAKA 25,MUWANJI MRISTO NA MKAZI WA IGAWILO   AKIWA NA BHANGI KETE 8 SAWA NA GRAMU  40 NDANI YA  MFUKO WA SURUALI . MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI HIYO .TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
Imesainiwa na,
 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Dunia Imeisha! 'Babu' mbaroni kwa kubaka 'vijukuu'


MBAKAJI ERASTO MWAKYOMO (50) ANAYETUHUMIWA KWA UBAKAJI AKIWA KATIKA OFISI YA MWENYEKITI WA MTAA WA MAPELELE KABLA YA KUCHUKULIWA NA MWENYEKITI WA DAWATI LA WATOTO NA UKATILI WA KIJINSIA MARY GUMBO.
WATOTO WALIOKUWA WAKIBAKWA WAKITOA MAELEZO JINSI WALIVYOKUWA WAKITENDEWA
 MWENYEKITI WA MTAA WA MAPELELE CHRISTOPHER MWAKIBETE AKIANDIKA BARUA KWA WAZAZI NA MTUHUMIWA KUPELEKWA POLISI 
 BAADHI YA WAZAZI NA NDUGU WA WATOTO WAKIWA NYUMBANI KWA MWENYEKITI WA MTAA.

***************

Ezekiel Kamanga

ERASTO MWAKYOMA mwenye umri wa miaka hamsini mkazi wa mtaa wa Mapelele Kata ya ILEMI jijini Mbeya anahojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwadhalilisha watoto wawili wa kike wote wakazi wa Mapelele.

Wazazi wa watoto hao baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watoto hao ambao mmoja ana umri wa miaka minne na mwingine mitano walitoa taarifa kwa Balozi wa mtaa Bwana CASIAN MWEZIMPYA ambapo baada ya kutafakari kwa kina aliamua kulipeleka suala hilo kwa Mwenyekiti wa Mtaa.

Mwenyekiti wa mtaa Bwana CHRISTOPHER MWAKIBETE Aliamua kuwaita wazazi na mtuhumiwa kuwahoji yaliyotukia ambapo nao watoto walipewa nafasi ya kueleza ambao walieza kuwa ERASTO Alikuwa akiwashika sehemu za siri na kuwapaka mafuta kabla ya kufanya nao mapenzi.

Baada ya kusikiliza kwa makini MWAKIBETE aliamuru kuwa suala hilo ni la kisheria na kitaalamu hivyo hawezi kuchukua hatua zozote bali suala hilo analazimika kulipeleka Polisi ambapo Mwenyekiti wa Dawati la watoto na jinsia MARY GUMBO Alimchukua mtuhumiwa hadi kituo cha Polisi kati.

Baada ya mahojiano ya awali GUMBO aliwachuchukua watoto hadi Hospitali ya Rufaa kwa uchunguzi na mtuhumiwa kubaki kituo cha kati kwa mahojiano zaidi,hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya watoto mtaani hapo wamekuwa wakitendewa vitendo vya ukatili lakini vimekuwa vikifumbiwa macho na baadhi ya wazazi wakihisi ni aibu kwa watoto wao.

 Na Mbeya yetu Blog

BREAKING NEWS!! UZEMBE WA TANESCO WASABABISHA KIFO CHA BINTI WA MIAKA 26 JIONI HII MBALIZI MBEYA

 HAPA NDIPO MAREHEMU ALIPOGUSA NA KUKUTWA NA MAUTI

NYAYA ZA UMEME AMBAZO ZIMENING'INIA MITA MOJA KUTOKA USAWA WA ARDHI ZIMESABABISHA KIFO CHA NEEMA B. KIPENYA (26) ALIPOTELEZA NA KUKAMATA NYAYA HIZO KISHA KUFARIKI PAPO HAPO.
 KATI YA NGUZO HADI NGUZO NI UMBALI WA ZAIDI YA MITA 75 MAHALI AMBAPO PALIPASWA KUWA NA NGUZO TATU LAKINI IKAWEKWA NGUZO MOJA , HALI MTEJA WA ENEO HILO ALIKUWA AMELIPIA NGOZO TATU ZAIDI YA MIAKA MIWILI ILIYOPITA .
 HAPA NDIPO ALIPO TELEZA MAREHEMU NEEMA NA KUANGUKIA NGUZO HIZO
 ASKARI AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MASHUHUDA 
 MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MSHIKAMANO BWANA KISMAN MWANGOMALE AMBAYE NDIYE MTEJA WA KWANZA KULIPIA TANESCO NGUZO TATU  NA KUFUNGWA NGUZO MOJA , NA AMETOA TAARIFA MARA KADHAA TANESCO NA HATA KUANDIKA BARUA KWA NIABA YA KIJIJI LAKINI HAKUNA UTEKELEZAJI ULIOFANYIKA HADI MADHARA YAMETOKEA NDIPO TANESCO WAMEFIKA.

MMOJA KATI YA WATUMISHI WA TANESCO AMBAYE ALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUKATA UMEME USILETE MADHARA ENEO HILO , HATA HIVYO ALINUSURIKA KUPIGWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI AMBAO WALIKERWA NA TUKIO HILO.

 MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MSHIKAMANO WA KWANZA KUSHOTO NA WATUMISHI WA TANESCO WAKIANGALIA NGUZO ZILIZO ELEMEWA NA UZITO WA NYAYA HIZO NA KUSABABISHA NGUZO KUSHINDWA KUHIMILI UZITO WA NYAYA HIZO. 
 WAOMBOLEZAJI WAKILIA KWA UCHUNGU KWANI MUDA MFUPI ULIOPITA WALIKUWA NA MAREHEMU NYUMBANI HAPO.
 MOJA KATI YA NDUGU AMBAYE ALIZIRAI KATIKA ENEO LA TUKIO
MWILI WA MAREHEMU UKIWA KATIKA CHUMBA CHA MAITI HOSPITALI YA IFISI ILIYOKO WILAYA YA MBEYA UKISUBIRI UCHUNGUZI ZAIDI WA KITABIBU.

PICHA NA EZEKIEL KAMANGA

SHEIKH PONDA ASOMEWA MASHITAKA AKIWA HOSPITALI

Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda amesomewa mashitaka ya uchochezi na Mwanasheria wa serikali, akiwa wodini MOI anapoendelea kupata matibabu. Sheikh Ponda arijeruhiwa Jumamosi iliyopita akiwa katika mhadhara wa Kiislamu huko mkoani Morogoro. Baada ya kujeruhiwa Ponda alilazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kuhamishiwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) aliposomewa mashitaka. Kesi yake itaendelea pindi atakapopata nafuu.

UCHAGUZI TFF SASA KUFANYIKA OKTOBA 18, USAJILI KUPITIWA IJUMAA


Na Boniface Wambura
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa tangazo la uchaguzi wa Kamati ya mpya ya Utendaji ambao utafanyika Oktoba 20 mwaka huu. Pia Kamati hiyo imetoa tangazo za uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPL Board) ambao utafanyika Oktoba 18 mwaka huu.

Akitangaza mchakato huo wa uchaguzi leo (Agosti 14 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni amesema nafasi zitakazogombewa kwa upande wa TFF ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.

Fomu kwa wagombea zitatolewa kuanzia Agosti 16 mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 kamili jioni kwenye ofizi za TFF. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti 20 mwaka huu. Fomu kwa nafasi ya Rais ni sh. 500,000, Makamu wa Rais ni sh. 300,000 wakati wajumbe ni sh. 200,000.

Mbwezeleni amesema kwa wale ambao walilipia fomu katika mchakato uliofutwa na wanakusudia kugombea nafasi zilezile walizolipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.

Kwa upande wa uchaguzi wa TPL Board, fomu zitaanza kutolewa Agosti 16 hadi 20 mwaka huu, na nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambapo ada ni sh. 200,000 wakati wajumbe wa Bodi ada ni sh. 100,000.

KAMATI YA SHERIA SASA KUPITIA USAJILI IJUMAA
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji iliyokuwa ikutane jana (Agosti 13 mwaka huu) na leo (Agosti 14 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza sasa itakutana keshokutwa (Agosti 16 mwaka huu) saa 4 asubuhi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Alex Mgongolwa amepanga tarehe hiyo mpya baada ya kikao cha jana kushindwa kupata akidi. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ina wajumbe saba, na ili kikao kiweze kufanyika ni lazima wapatikane wajumbe kuanzia wanne.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)