STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 18, 2013

Fike, J-Plus sasa wanasa kwa Jamali

Fike Wilson akiwa na mkewe Irene Wambura
BINGWA wa zamani wa kutunisha misuli nchini, Fike Wilson 'Wild Cat', amevunja ukimya kwa kuibuka na filamu mpya iitwayo 'Jamali'.
Filamu ya Fike inakuja baada ya kupita miaka karibu miwili tangu msanii huyo alipofyatua kazi yake ya mwisho iitwayo 'Lost Dream'.
Fike alisema kwa sasa yupo katika hatua ya mwisho kabla ya kuiachia mtaani filamu hiyo ambayo imewashirikisha wasanii kadhaa nyota.
"Nipo katika maandalizi ya kuiachia sokoni filamu yangu mpya iitwayo 'Jamali' ambayo ilikamilika tangu mwaka jana ila nilichelewa kuitoa,": alisema.
Fike alisema katika filamu hiyo ya 'Jamali', ameigiza na wasanii kadhaa wanaotamba nchini kama Jimmy Mponda 'J Plus', Ahmed Olotu 'Mzee Chillo', Mobby Mpambala na Irene Wambura 'Maurine'.
"Ni filamu tangu pengine kuliko kazi zangu zote za nyuma kama Power of Love, Lost Dream na nyingine, kutokana na wasanii walioshiriki katika filamu hiyo mpya ya Jamali," alisema Fike.
Fike alisema wakati akijiandaa kuiingiza mtaani filamu hiyo tayari ameshakamilisha kazi nyingine mpya ambayo hata hivyo aliomba isitajwe kwa sasa ili awashtukize mashabiki wake baadaye atakapoitoa.

 

LIVERPOOL YAZINDUKA EPL, YAPIGA MTU 5-0

Steven Gerrard akifunga penati na kuipa uongozi Liverpool jana

LIVERPOOL jana ilizinduka kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuipa kipigo kitakatifu timu ya Swansea City wa kuifunga mabao 5-0 katika pambano pekee la ligi hiyo lililochezwa jana kwenye uwanja wa Anfield.
Nahiodha Steven Gerrard alianza kuiandikia bao Liverpool katika ya 34 kwa mkwaju wa penati bao lililodumu hadi wakati wa mapumziko.
Vijana hao wa Brandts Rodgers, kocha aliyekuwa akiinoa Swansea kabla ya kutua Liverpool msimu huu, waliongeza mabao mengine katika kipindi hicho cha pili kupitia Philippe Coutinho aliyefunga dakika ya 46 akimalizia kazi nzuri ya Luis Suarez, kabla ya dakika tano baadaye José Enrique kufunga bao la tatu.
Dakikia ya 56, Suarez alifunga bao la nne na Daniel Sturridge kuhitimisha karamu ya mabao kwa mkwaju wa penati dakika ya 71 na kuifanya Liverpool kupata ushindi wa kwanza katika mechi tano ilizocheza hivi karibuni.
Mechi tatu zilizopita timu hiyo iliambulia sare mbili na kipigo toka kwa West Bromwich, huku pia wakinyukwa katika michuano ya Kombe la Ligi ya Ulaya na Zenith.
Kwa ushindi huo LIverpool imechupa  kutoka nafasi ya tisa hadi ya saba ikiwa na pointi 39.