STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, October 31, 2013

TASWA WAPONGEZA UONGOZI MPYA WA TFF

 
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kinatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliochaguliwa Jumapili iliyopita.
 
Tunaungana na wapenda michezo na Watanzania kwa ujumla kuitakia kila la heri Kamati ya Utendaji ya TFF na shirikisho hilo kwa ujumla chini ya Rais mpya Jamal Malinzi na Makamu wake, Wallace Karia.
 
TASWA inaamini Malinzi, Karia na wajumbe wao ni wazoefu na ni watu wenye kujua mambo mengi yanayohusu mpira wa miguu nchini, hivyo tunaamini watakuwa viongozi wazuri kwa nafasi zao katika kuhakikisha shirikisho hilo linasonga mbele.
 
Tunawatakia kila la heri Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji, huku tukiamini hawatawaangusha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF waliowaamini kushika nafasi hizo.
 
TASWA na waandishi wa habari za michezo kwa ujumla hapa nchini tunaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha ili watekeleze majukumu yao ipasavyo.
 
Nawasilisha.
 
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
30/10/2013

Mtanzania kuwania ubingwa wa Dunia wa WBC

Bondia Omer Kimweri
BONDIA Mtanzania anayefanya shughuli zake nchini Australia, Omari Kimweri 'Lion Boy' anatarajiwa kuwa Mtanzania wa kwanza kupanda ulingoni kuwania taji la Dunia la WBC katika pambano litakalofanyika Novemba 30.
Kimweri atapanda ulingoni katika pambano la uzito wa Minimum (kilo 47.5) nchini China kupigana na bingwa mtetezi wa taji hilo duniani, Mchina Xiong Zhao Zhong.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotumwa kwa MICHARAZO, Kimweri amepata nafasi ya kupigana na Zhong kutokana na rekodi nzuri aliyonayo katika mchezo huo akiwa amepanda ulingoni mara 16 na kushinda michezo 13.
Kati ya michezo hiyo Mtanzania huyo amepoteza michezo mitatu tu, wakati mpinzani wake amecheza michezo 26 na kushinda 21 na kupigwa michezo minne na mmoja kuambulia sare hali inayoonyesha pambano hilo litakuwa kali.
"Kura zilimuangukia Kimweri baada ya kutakiwa bondia kutoka Afrika mwenye rekodi nzuri kupambana na bingwa huyo wa dunia wa WBC Minimum Weight, hivyo Kimweri anakuwa Mtanzania wa kwanza kuwania taji hilo," taarifa hiyo ilisomeka hivyo.
Mara ya mwisho kwa Mtanzania huyo kupanda ulingoni ilikuwa Julai 25 mwaka huu ambapo aliibuka na ushindi wa TKO ya raundi ya kwanza.
Kimweri yupo kwenye mazoezi makali akifanyishwa akisaidiwa na bondia bingwa wa Lightfly kutoka Ufilipino, Randy Petalcoria.

Wednesday, October 30, 2013

Majaji kutoa uamuzi wa hukumu ya kesi ya Babu Seya na mwanae

 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo. Nguza na Papii walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na ulawiti. (Picha zote: Francis Dande)


 Watu waliohudhuria mahakama hapo wakifuatilia kesi hiyo.


 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.  


 Mahakamani.


Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza wakiteta jambo na wakili wao, Mabere Marando.

 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza 'Papii' wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia hukumu iliyoitoa mwaka 2010.


 Nyuso za matumaini.......


 Johnson  Nguza 'Papii' akibusu mkono wake baada ya kuibusu ardhi mara baada ya kutoka mahakamani.


 Papii akinyoosha mkono juu kama ishara ya kumshukuru mungu.


 Waandishi wa habari wakiwa chini wakati wa harakani za kuchukua matukio mahakamani hapo.




 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza wakati wakitoka mahakamani.

Yanga, Mgambo waingiza kiduchu!

PAMBANO la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mgambo Shooting lililochezwa jana (Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 37,915,000.
Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 46 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 walikuwa 6,515 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 5,783,644.07, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,145,790 wakati kila klabu ilipata sh. 8,550,741.95.
Wamiliki wa uwanja walipata sh. 4,347,834.89, gharama za mchezo sh. 2,608,700.93, Bodi ya Ligi sh. 2,608,700.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,304,350.47, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,014,494.81.