Mary Mbosa aliyenusurukia kuchinjwa na mtalaka wake na kulzaimika kuishi porini kama mkimbizi. |
Na Gustav Chahe, Iringa
MAMA mmoja mkazi wa Itunundu – Pawaga katika Mkoa wa Iringa Mery
Mbosa anaishi kama digidigi baada ya kunusurika mara kadhaa kuchinjwa na
mtalaka wake na kulazimika kuhama kijiji kwa ajili ya kunusuru maisha.
Akiongea na mtandao huu jana, Bi Mbosa alisema maisha yake yapo
hatarini kutokana na kuvamiwa na mtalaka wake mara kadhaa akiwa nyumbani
na kumuumiza.
Alisema alilazimika kutalakiana baada ya mwanamume huyo kuwa mkorofi
kiasi cha kupigwa, kutokuwa huru kutumia mazao ambayo walilima wote na
hata kutokuwa huru kuongea na watu hata kama ni ndugu zake kwa madai
kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Alisema mtalaka wake amegeuka kuwa mnyama na kufika nyumbani kwake
usiku wa manane na pindi anapokuta mlango umefungwa huanza kurusha mawe
madirishani huku akitaka kuvunja mlango ili kuingia kumdhuru.
Amemtaja mtalaka wake kuwa ni Phabiani Msilamgunda ambaye miezi ya
hivi karibuni alikutana na ye njiani akielekea shambani akamvamia akiwa
na kisu kwa kutaka kumchinja na kuokolewa na watu ambao walikuwa jirani.
“Ilikuwa 23 Machi mwaka huu nilikuwa nikielekea shambani nikakutana
na mtalaka wangu akiwa na kisu mkononi akanivamia huku akisema
nakuchinja laeo lakini kwa bahati nzuri kulikuwa na watu jirani
wakaniokoa vinginevyo ningekuwa marehemu.
“Lakini hata hivyo amekuwa akimtukana hata mama yangu mzazi (mama
mkwe) akitaka kupiga pia na kila wakati nimekuwa nikishtaki hadi ofisi
zinanichoka pamoja na kuwa ninapokelewa na akiitwa haendi kwa sababu
amekuwa mbabe” alisema bi Mbosa.
Hata hivyo Mbosa alisema kuwa aliwahi kupigwa na kuumizwa vibaya na
kulazimika kushtaki mahakamani japo kuwa hukumu ilivyotolewa haikuwa ya
haki na kuhatarisha zaidi maisha yake.
“Nilipigwa na kuumizwa vibaya kesi ikapelekwa mahakamani lakini
hukumu ilivyotolewa haikuwa ya haki kwangu na baada ya hukumu maisha
yangu yamekuwa ni ya hatari zaidi” alisema.
Kwa mujibu wa maelezo ya wananchi wa kijiji hicho ambao wameeleza
kushuhudia mama huyo akinusurika kuuawa na jinsi maisha yake yanavyozidi
kuwa mabaya, walisema kiburi cha Msilamgunda kinatokana na dada yake
ambaye ni diwani wa viti maalum (CCM).
Gazeti hili limebaini kesi ambayo mama huyo hajaridhika na hukumu ni
Jinai No. 22/2013, mshitakiwa Phabiani Msilamgunda ambayo ilitolewa
hukumu Mei 21 Mwaka huu.
Imeelezwa kuwa katika utoaji huku hiyo hakimu aliyetajwa kwa jina
moja la Masuwe alimtaka mtuhumiwa alipoe faini ya shilingi laki mbili
pamoja na gharama ya
kesi shilingi 45 elfu jambo ambalo lilifanyika
hivyo na mtuhuhumiwa kuwa huru kwa vitisho kuwa lazima ammalize mwanamke
huyo.
Pamoja na kutokuridhika na hukumu iliyotolewa, Mkuu wa kituo cha
Polisi cha Pawaga Fedrick Nyavilwe anatuhumiwa kumdhurumu mama huyo na
kuiomba serikali kumsaidia ili aishi kama wanavyoishi wananchi wengine.
Nyavilwe anatuhumiwa kumdhurumu mwanamke huyo mbegu ya mpunga na
kumfanya kuwa mtumwa kwa kukosa chakula bila kujua hatima ya maisha
yake.
“Baada ya hukumu nilikwenda shambani nilikokuwa ninaanda mbegu ya
mpunga kwa ajili ya kupanda nikakuta watu wananing’oa, nilipouliza
walisema wametumwa na Mkuu wa kituo cha polisi. Hivi sasa naishi kama
ndege jamani sijui nitakula nini kwa sababu hata mashamba niliyokuwa
nalima nilinyang’anywa na mbegu niliyokuwa nimeandaa kwa ajili ya
kupanda polisi wameninyang’anya” alisema.
Alipotafutwa kwa njia ya simu kwa ajili ya kutolea maelezo, Veronica
Msilamgunda ambaye ni ndugu na Phabian Msilamgunda alisema hawezi
kuzungumza chochote kwa kuwa yupo kwenye mkutano.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Joseph Malinga
alipotafutwa kwa ajili ya ufafanuzi Alikiri kuwa mama huyo ni mhanga
mkubwa na anaishi kama mkimbizi kwa hofu ya kuuawa.
“Nalijua sana hilo na ninashukuru kwa kuwa umenitafuta ili nikueleze.
Maisha ya huyo mama hatuji yataishia wapi kwa sababu hali ilivyo kwa
sasa ni ngumu na anaishi kama mkimbizi.
“Hata akiwa sehemu yenye ulinzi anaona kama hakuna ulinzi kwa sababu
ya kile anchofanyiwa. Kiujumla hata sisi viongozi wa kijiji tunaishi kwa
mashaka kwa sababu tunatishiwa kuuawa tunapotaka kutafutas suluhu ya
huyo mama. Huyu mwanaume tunashindwea kuelewa kama ni mtu wa kawaida
maana amegeuka kuwa kamas samba” alismea Malinga.
Hata hivyo alisema anaomba kwa watu wanaoweza kumsaidia mama huyo
kupata hifadhi ili aondokane na maisha ya kuishi kama digidigi kule
kijijini.
No comments:
Post a Comment