STRIKA
USILIKOSE
Sunday, June 2, 2013
Taifa Stars, Sudan zashindwa kutambiana Ethiopia
TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars jioni hii imetoshana nguvu na Sudan katika pambano la kimataifa la kirafiki lililochezwa mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia ilipoweka kambi yake ya kujiandaa na michuano ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazili.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura Stars ilionyesha uwezo mkubwa licha ya kuchezesha vijana katika pambano hilo kwa nia ya kuwapa uzoefu zaidi katika kikosi hicho ambacho kwa sasa wapo kwenye hafla nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
Kikosi hicho kitaondoka kesho nchini Ethiopia kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda Morocco kwa kupitia Misri ili kukwaruzana na wenyeji wao katika pambano la marudiano la kundi C kwa nia ya kuwania kucheza fainali hizo za Brazili.
Katika mechi ya kwanza Stars iliinyuka Morocco mabao 3-1 na ushindi huo iliifanya Stars kuendelea kusalia nafasi ya pili ikijikusanyia pointi 6, moja nyuma ya Ivory Coast yenye pointi saba ambayo nayo wikiendi ijayo itakuwa dimbani klupambana na Gambia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment