STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 4, 2013

Azam watua salama Sauzi kuivaa Kaizer Chiefs kesho

Wachezaji wa Azam wakijiandaa kuanza mazoezi nchini Afrika Kusini

KLABU ya soka ya Azam imetua salama nchini Afrika Kusini na imeanza kujifua kwa mazoezi ya kambi yao na panapo majaliwa kesho itashuka dimbani kuvaana na Mabingwa wa nchini humo, Kaizer Chiefs katika pambano lao la kwanza kati ya manne itakayocheza huko.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu hiyo, Jafar Idd alisema kuwa timu hiyo imefika salama na kwamba vijana wao walishaanza mazoezi kwa ajili ya mechi ya kesho itakayochezwa jioni.
Jafar alisema baada ya mechi ya kesho timu yao itapumzika siku moja kabla ya kurudi tena dimbani kuvaana na Orlando Pirates kisha kukwaruzana na Mamelodi Sundowns na kumalizia ziara yao Agosti 12 dhidi ya Moroka Swallows.
Mechi yao ya kesho itachezwa kituo cha mazoezi cha kaizer kitwacho Machorena na Meneja wa timu hiyo ya Azam, Jemedari Said amenukuliwa akisema kuwa kambi yao ipo katika hadhi ya hali ya juu kuwawezesha kujiweka vyema kwa michuano iliyopo mbele yao ikiwamo Ligi Kuu na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayoshiriki kwa marea ya pili mfululizo mwakani.

No comments:

Post a Comment