Ige Moyaba aliyerejea tena Twanga atatambulishwa Idd Pili |
Mkurugenzi
wa bendi hiyo Asha Baraka alisema jana kuwa onyesho hilo limeandaliwa na Bob
Entertainment na kudhaminiwa na Konyagi, Freddito Entertainment, Saluti5 na
Twitter Pub.
Alisema
wanamuziki watakaotambulishwa siku hiyo maalum ni wanenguaji wapya, muimbaji Ige
Moyaba ambaye alikuwa mwanamuziki wa bendi hiyo kabla kwenda Ufaransa kuendeleza
kipaji chake.
“Tumeamua kuleta wanenguaji wapya kabisa, wenye
damu changa ili kuleta mapinduzi kwenye muziki wa dansi. Madansa wetu ni
mabinti warembo, pia tuna wanenguaji watanashati,”
alisema Asha na kuongeza kuwa awameamua kubadilisha wanenguaji ili kuenda na
wakati pamoja na soko la muziki.
Kwa upande
wa Ige Moyaba aliyetamba kwenye albamu ya ‘Mtu
Pesa’ katika mwaka wa 2004, Asha
alisema ameanda vitu vipya kuwapa mashabiki wa bendi hiyo inayotamba kwa staili
ya Kisigino.
“Kwa kweli
hi siyo onyesho la kukosa kwani itakuwa ni zawadi yetu ya Idd kwa mashabiki
wetu,” mkurugenzi huyo alisema.
Mwezi
uliyopita Twanga Pepeta walizindua albamu yao ya 10 lijulikanayo kana “Nyumbani
ni Nyumbani”.
Albamu
zingine ambazo zitapigiwa siku hiyo ni Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binafsi,
Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa, Safari, Password, Mtaa Wa Kwanza, Mwana Dar es Salaam na
Dunia Daraja.
Naye mratibu
wa onyesho hilo Joseph Kapinga alisema kuwa warembo watakoshiriki kwenye
shindano la kumtafuta Redds Miss Ilala pia watatambulishwa siku hiyo.
BENDI ya
African Stars “Twanga Pepeta” itatambulisha wanamuziki wapya pamoja na warembo
watakaoshiriki Miss Ilala siku ya Iddi Pili Katika ukumbi wao wa Mango Garden,
Kinondoni.
Mkurugenzi
wa bendi hiyo Asha Baraka alisema jana kuwa onyesho hilo limeandaliwa na Bob
Entertainment na kudhaminiwa na Konyagi, Freddito Entertainment, Saluti5 na
Twitter Pub.
Alisema
wanamuziki watakaotambulishwa siku hiyo maalum ni wanenguaji wapya, muimbaji Ige
Moyaba ambaye alikuwa mwanamuziki wa bendi hiyo kabla kwenda Ufaransa kuendeleza
kipaji chake.
“Tumeamua kuleta wanenguaji wapya kabisa, wenye
damu changa ili kuleta mapinduzi kwenye muziki wa dansi. Madansa wetu ni
mabinti warembo, pia tuna wanenguaji watanashati,”
alisema Asha na kuongeza kuwa awameamua kubadilisha wanenguaji ili kuenda na
wakati pamoja na soko la muziki.
Kwa upande
wa Ige Moyaba aliyetamba kwenye albamu ya ‘Mtu
Pesa’ katika mwaka wa 2004, Asha
alisema ameanda vitu vipya kuwapa mashabiki wa bendi hiyo inayotamba kwa staili
ya Kisigino.
“Kwa kweli
hi siyo onyesho la kukosa kwani itakuwa ni zawadi yetu ya Idd kwa mashabiki
wetu,” mkurugenzi huyo alisema.
Mwezi
uliyopita Twanga Pepeta walizindua albamu yao ya 10 lijulikanayo kana “Nyumbani
ni Nyumbani”.
Albamu
zingine ambazo zitapigiwa siku hiyo ni Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binafsi,
Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa, Safari, Password, Mtaa Wa Kwanza, Mwana Dar es Salaam na
Dunia Daraja.
Naye mratibu
wa onyesho hilo Joseph Kapinga alisema kuwa warembo watakoshiriki kwenye
shindano la kumtafuta Redds Miss Ilala pia watatambulishwa siku hiyo.
No comments:
Post a Comment