Lori
lenye namba za usajili T97 AJL lenye tela namba T746 BKF lilipo acha njia na
kupinduka na kuziba njia
Lori
likishindwa kupita baada ya Mafuta kumwagika Barabarani na kusababisha barabara
kushindwa kupitika
Magari
yakipita kwa shida baada ya Lori kudondoka
Askari
wakijitahidi kukabiliana na watu waliokuwa wanachota mafuta
Shughuli
za uokoaji zikiendelea kulia ni Dereva wa Lori hilo baada ya
kunusurika
Dereva wa
gari hilo Hassan Abdi (35) akiwa haamini kilicho tokea baada ya Kunusurika
kifo
YALE
YALE!!! Wananchi wenye ndooo Haya.... Wenye Madumu haya .... wenye Masefuria
haya... wote walikuwepo kuchota Mafuta kama inavyo onekana ... bila kujali kama
yaweza kulipuka
Wananchi
Mbalimbali wakiwa wanapata shida kupita baada ya Lori kudondoka
Askari wa
zima moto wakiwa wanaendelea na Juhudi za kuondoa mafuta barabarani kwa
maji
Wananchi
mbalimbali wakiwa wanaondoka na Mafuta... huku wengine wakiendelea
kuchota
Wakina
mama... Watoto... Vijana na wazee wakiwa wanapata shida jinsi ya kupita baada ya
ajali
Kushoto
ni Tingo Saimoni Msovela (23) na dereva wake Hassan Abdi wakijitahidi kuziba
mafuta yasiendelee kuvuja
veta
Tingo wa
Lori hilo la mafuta baada ya kuokolewa kutoka kwenye Gari.
Ezekiel
Kamanga
WATU
wawili wamenusurika kifo baada ya lori la mafuta lenye namba za usajili T 978
AJL lenye tela namba T 746 BKE Aina ya SCANIA walilokuwa wakisafiria kutoka DAR
ES SALAAM kwenda ZAMBIA kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa MBALIZI
barabara MBEYA TUNDUMA.
Dereva
ametambuliwa kwa jina la HASSAN ABDI 35 na msaidizi wake SAIMON SOVELA 23 ambao
walikuwa wametokea DAR ES SALAAM kuelekea ZAMBIA likiwa limejaa shehena ya
mafuta
Kwa
mujibu wa Dereva amesema kuwa gari hilo ghafla lilipoanza kuteremka mteremko
liliharibika mfumo wa breki na mbele yake kukiwa na magari matano baada ya kuona
kuwa angesababisha maafa makubwa aliamua kulichepusha pembeni ndipo lilipoacha
njia na kupinduka na kumwaga shehena ya mafuta.
Kikosi
cha zimamoto kilifika eneo la tukio na kuhakikisha usalama wa eneo hilo kuhofia
mlipuko wa moto ambao ungeweza kutokea kutokana na baadhi ya wananchi kuanza
kuchota mafuta yaliyokuwa yanatiririka.
Pamoja na
juhudi za Jeshi la Polisi kudhibiti wananchi kutochota mafuta lakini wananchi
walikaidi na kuendelea kuchota mafuta.
Ajali
hiyo ilisababisha adha kubwa kwa wasafiri waliokuwa wana pita barabara hiyo
wakiwemo wagonjwa na waliokuwa wanawahi usafiri wa ndege majira ya saa saba
mchana.
No comments:
Post a Comment