STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 4, 2013

Bahanuzi, Javu waizamisha Mtibwa Sugar Taifa

 Beki wa Mtibwa Sugar, Salvatory Ntebe akichuana na mshambuliaji wa Yanga wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga imeshinda 3-1. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
 Beki wa Mtibwa Sugar, Ally Lundega akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
 Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Ramadhan wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 


 Kikosi cha Mtgibwa Sugar.
Kikosi cha Yanga.
 Mashabiki wa Yanga waklifuatilia mtanange huo.

Young Africans leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wakata miwa kutoka Morogoro timu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu uliofanyika katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ikiwatumia wachezaji wake wapya iliyowasajili kwa ajili ya msimu huu kikosi cha mholanzi kiliingia uwanjani kwa lengo la kuhakikisha wanapata ushindi na kuendeleza heshima kwa timu wanazokutana nazo.
Dakika ya sita ya mchezo mshambuliaji mpya Shaban Kondo almanusura aipatie Young Africans bao baada ya kupokea krosi safi ya Said Bahanuzi kutoka upande wa kulia lakini kutokua makini kwa mshambuliaji huyo kulimfanya mlinda mlango wa Mtibwa Sugar Hussein Sharrif kuokoa hatari hiyo.
Said Bahanuzi aliwainua washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Yanga dakika ya 24 ya mchezo baada ya kuukwamisha mpira wavuni kufuatia mlinzi wa mtibwa kuokoa kwa kichwa mpira wa Jerson Tegete ulikokuwa ukielekea wavuni.
Mara baada ya bao hilo Mtibwa Sugar waliongeza kasi ya mashambulizi kwa lango la Yanga ili waweze kupata bao la kusawazisha laikini harakatia zao zilishia mikononi mwa mlinda mlango Deogratius Munishi 'Dida' 
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 1 - 0 Mtibwa Sugar.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo Yanga iliwaingiza golikipa Ally Mustapha 'Barthez, Rajab Zahir, David Luhende, Bakari Masoud, Hussein Javu, na Abdallah Mguhi 'Messi, mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya mchezo.
Dakika ya 57 ya mchezo Shaban Kisiga aliipatia Mtibwa Sugar bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinzi Rajab Zahir kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na Kisiga kufunga penati hiyo na kupata bao la kusawazisha.
Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 80 ya mchezo kufuatia mlinzi wa kati wa Mtibwa Sugar Salvatory Ntebe kumkwatua Tegete na mwamuzi kuamuru penati ambayo aliipiga Tegete na kuukwamisha mpira wavuni.
Huku washabiki wa soka wakianza kutoka nje na wengine wakiwahi kufuturu Hussein Javu aliifungia Yanga bao la tatu na la ushindi dakika ya 87 ya mchezo kufuatia mpira aliorudhishiwa golikpa Said Mohamed kushindwa kuuondoa na Javu kuuwahi na kuhesabu bao la tatu kwa watoto jangwani.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 - 1 Mtibwa Sugar.
Mara baada ya mchezo kocha mkuu wa Yanga Ernie Brandts amesema kikosi chake kinaendelea kuimarika na wachezaji wanaonekana kushika vizuri mafunzo yake, anaendelea na mazoezi kwa hizi wiki mbili kabla ya kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya timu ya Azam FC Agosti 17 2013.
Young Africans: 1.Deogratius Munishi 'Dida'/Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua/David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro'/Rajab Zahir, 5.Issa Ngao, 6.Athuman Idd 'Chuji/Bakari Masoud, 7.Said Bahanuzi/Abdallah Mguhi 'Messi', 8.Salum Telela, 9.Jerson Tegete, 10.Shaban Kondo/Hussein Javu, 11.Haruna Niyonzima.

No comments:

Post a Comment