Juma kaseja akiwa kando yawatoto yatima |
Wachezaji wa Golden Bush wakiwa pamoja na yatima hao |
Mmoja wa wachezaji wa Golden Bush akiwa amebeba mmoja wa yatima hao |
Watoto wakifurahia kujumuika na wachezaji wa Golden Bush |
Naondoka na wewe! Yatima akiwa mikononi mwa mmoja wa wachezaji wa Golden Bush |
Salum Swedi akizungumza jambo, kushoto KR Mulla na kulia kwake ni Herri Morris |
Yatima wa kituo cha New Life Orphans Home wakiimba wakati wachezaji wa Golden Bush walipowatemebelea leo |
Katibu wa kituo cha Kulelea Yatima cha New Life Orphans Home, Hamad Kombo (kushoto) akisoma risala fupi mbele ya uongozi wa Golden Bush |
Yahya Issa kati akiwa amempakata mtoto kando ya Mkuu wa Nidhamu wa kituo cha kulelea Yatima Mbwana Said huku Herry Morris akiwa kando yake kushoto |
Rashid Ziada 'KR Mullah' naye alikuwa mmoja wa wana Golden Bush waliotembelea kituo cha yatima na kuwaonyesha namna ya kucheza Mapanga Shaa' |
Msaada huo Golden Bush ulitolewa leo asubuhi na wachezaji hao wakiongozwa na mlezi wao, Onesmo Waziri 'Ticotico', viongozi na nyota kama Juma Kaseja, Salum Swedi 'Kussi' , Yahya Issa, Amani Simba, Waziri Madhi na wengine una thamani ya Sh. 3.5.
Baadhi ya msaada huo ni sabuni, juisi, mchele, sukari, mafuta ambavyo vilikabidhiwa na timu hiyo kwa uongozi wa kituo hicho ukiongozwa na Katibu Mkuu wake, Hamad Kondo na Mkuu wa Nidhamu, Mbwana Said.
Yatima hao wakiwa na bashasha na hasa baada ya kuwaona wachezaji hao mastaa waliwaimbia Golden Bush na kuchezewa miondoko ya Mapanga Shaa na msanii Rashid Ziada 'KR Mullah' ambaye naye ni mchezaji wa timu hiyo kabla ya Katibu wa kituo kusoma risala fupi.
Hamad akieleza kwa ufupi kwamba historia ya kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2001......kikiwa na watoto 17 tu tofauti na sasa wanafikia 103 wasichana wakiwa 38 na waliosalia wakiwa ni wavulana.
Katibu huyo alieleza kuwa kituo chao kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ada za kuwalipia wanafunzi wanaosemeshwa na kituo hicho ambapo baadhi wapo Shule ya Msingi na wengine wa Sekondari.
Pia Hamad aliweka bayana kuwa kituo chao kimefanikiwa kupata eneo huko Boko-Dawasa na wamejenga jengo la ghorofa moja ambalo walisaidiwa kiwanja na mlezi wao na mpaka sasa jengo hilo limesimama isipokuwa bado halijamalizika kutengenezwa sakafu.
Mlezi wa Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' akizungumza kabla ya kuupisha uongozi wa juu wa timu hiyo, alisema wanafahamu walichokitoa ni kidogo, lakini waliuomba uongozi upokee kwa mikono miwili na kuahidi kutoa msaada wa kifedha kupitia akaunti ya kituo hicho.
"Nimesikia kilio chenu, ninachoomba nipeni namba yenu ya akaunti nami nilichojaliwa nitakituma huko, ila kwa sasa tunaomba mpokee japo hiki kidogo kwa ajili ya kuwafariji watoto katika kuelekea sikukuu ya Eid," alisema Ticotico.
Nao Mwenyekiti wa timu hiyo, Salum Swedi na Katibu wake, Herry Morris waliwataka watoto hao kuwa watiifu na kuishi kwa wema na Mungu akiwajalia waje kuwa nyota kama walivyokuwa wao katika soka, huku wakijinadi wapo wanaodaka kama Kaseja ambaye walimshangilia zaidi na kuonyesha kumjua na kutaka kupiga naye picha kila mara.
Naye Kaseja alipata nafasi ya kuzungumza na watoto hao na kuwataka kujibidiidha katika masomo, kumcha Mungu na kuwa watiifu kwa kila mtu na kwa wale wenye vipaji waviendeleze ili vije kuwasaidia ukubwani kama ilivyokuwa kwake na wenzake waliowatembelea.
No comments:
Post a Comment