STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 4, 2013

Watanzania wahimizwa kuwasaidia yatima kila mara badala ya sikukuu tu

Mlezi wa timu ya Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' akizungumza baada ya kukabidhi msaada katikia kituo cha kulelea yatima cha New Life Orphans Home mapema leo (Agosti4) Wengine picha mezani toka kushoto ni Katibu wa Golden Bush, Herri Morris, Katibu wa kituo hicho, Hamad Kombo na Abuu Ntiro ambaye ni miongoni mwa viongozi wa timu hiyo.

Baadhi ya misaada iliyotolea na Golden Bush (mwenye shati la mistari) ni nyota wa zamani wa Yanga na Reli, Yahya Issa

Katibu wa Golden Bush, Herri Morris akizungumza huku viongozi wenzake 'Ticotico na Abuu Ntiro wakiwa makini.

Juma Kaseja akiwa katika picha ya yatima wa kituo cha New Life Orphans Home. Kipa huyo alikuwa kivutio kwa watoto hao ambapo hakuhitaji kujitambulisha kwani watoto walisema wanamjua kuwa ni JK wa Taifa Stars
Ticotico (mwenye miwani) pamoja na wachezaji wa Golden Bush wakiwa katika picha ya pamoja na yatima wa kituo cha New Life Orphans Home cha Kigogo walipoenda kuwapa msaada wenye thamni ya Sh Laki 3.5.
WATANZANIA wamehimizwa kuwasaidia yatima kila mara wapatapo nafasi badala ya kusubiri kufanya hivyo kipindi cha sikukuu kwa kugawa misaada kwa kile kinachoelezwa watoto hao hawahitaji katika kipindi hicho tu bali kila siku kutokana na kukosa wazazi na walezi wa kuwalea kama watoto wengine.
Wito huo umetolewa na Mlezi wa klabu ya Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' wakati walipokitembelea na kutoa msaada katika kituo cha kulelea yatima cha New Life Orphans Home, kilichopo Kigogo Dar es Salaam.
Ticotico alisema yatima ni wahitaji wa kila siku hivyo ni vyema jamii ikawa na utamaduni wa kujitolea kuwasaidia kila mara badala ya kusubiri vipindi vya sikukuu kana kwamba wakati huo pekee ndipo watoto hao hula na kunywa au kuhitajia misaada zaidi.
"Huu umekuwa kama utamaduni kila wakati wa sikukuu kama za Pasaka, Krismasi au Idd ndipo utaona watu wakipigana vikumbo kuwasaidia yatima, huu sio utamaduni mzuri, watoto hawa wanahitaji misaada kila siku hivyo jamii iwe inawatupia macho kuwafanya wajihisi vyema na kufarijika," alisema.
Alisema ingawa hiyo ni mara yao ya kwanza kukitembelea kituo hicho, lakini klabu yao ya Golden Bush imekuwa na kawaida ya kufanya hivyo kwa vituo vingine na wakati kwa siri kwa kutambua jukumu la kuwasaidia yatima ni la kila mtu na yeye kama mwanajamii anawajibika kufanya hivyo kwa siri na dhahiri.
Ticotico alisema anaamini kuwasaidia watoto hao kunawafanya wasijisikie vyema na kujiona kama watoto wengine na kuahidi kuwa bega kwa bega na kituo hicho baada ya kuelezwa matatizo yao ikiwemo kutaka kumalizia jengo lao lililopo Boko-DAWASA.
Naye Katibu wa kituo hicho alishukuru msaada huo uliopelekwa kituoni hapo na wachezaji wa timu hiyo wengi wao wakiwa ni mastaa wa kandanda nchini kama akina Juma Kaseja, Salum Swedi, Abuu Ntiro, Salum Athuman 'Majani', Herry Morris, Aman Simba, Kudra Omar, Wazir Mahadhi na wengine.

No comments:

Post a Comment