Aliyekuwa beki wa kulia wa timu ya Rhino Rangers ya Tabora, Amani Juma kulia akisaini mkataba wa kipindi cha miaka miwili kuitumika timu hiyo katika msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kushoto ni katibu
Mkuu wa Coastal Union Kassim El Siagi.Aliyekuwa beki wa kati wa timu ya Mgambo Shooting ya Tanga,Bakari Mtama akisaini mkataba wa kuijunga na timu ya Coastal Union ya Tanga jana wanaoshuhudia katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto wa kwanza kulia ni Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi na wa pili kushoto ni mjumbe wa kamati ya usajili wa klabu hiyo, Salim Amiri.

Mshambuliaji Mpya wa timu ya Coastal Union,Husein Sued akisaini mkataba wa mwaka mmoja wa kujiunga na timu hiyo yenye makazi yake barabara ya kumi na moja jijini wanashuhudia katikati ni Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi na wa kwanza kulia ni Meneja wa timu hiyo, Akida Machai.
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
BEKI wa Kulia wa timu ya Coastal Union,Amani Juma amesema atahakikisha
anashirikiana na wenzake ili kuweza kuipa mafanikio timu hiyo katika
michuano ya Ligi kuu Tanzania bara lengo likiwa kuiwezesha kuchukua
kombe hilo na kuweza kushiriki mashindano makubwa.
Juma ambaye alisajiliwa na Coastal Union kwa mkataba wa miaka miwili
alisema ni wajibu wake kujituma na kupambana vilivyo kuiwezesha timuhiyo kufikia malengo yao waliojiwekea msimu ujao ya kumaliza ligi hiyo
wakiwa mabingwa.
Alisema katika kutimiza suala hilo wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo hawana budi kushikamana na kuwa kitu kimoja kwa kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mechi zao za nyumbani na ugenini wakati ligi
hiyo itakapoanza.
Aidha aliwashukuru viongozi wa klabu hiyo kwa kuthamini mchango wake
kwa kumpa ridhaa ya kuichezea timu hiyo katika kipindi hicho na kuahidi kupambana kufa na kupona kwa ajili ya kufikia mafanikio
yatokanayo na soka hilo.
Katika hatua nyingine wachezaji wote waliosajiliwa na timu hiyo
wanatakiwa kuwasili mkoani Tanga Kesho(leo) kwa ajili ya kuanza
maandalizi ya kuelekea msimu mpya bila kukosa kwani watakaochelewa kuwasili watachukuliwa hatua za kinidhamu.

No comments:
Post a Comment