Hiyo imethibitishwa na timu iliyoonyesha soka la kusisimua nchini Brazil, Algeria iliyong'oka kishujaa mbele ya Ujerumani.
Mshambuliaji nyota wa
timu ya taifa ya Algeria Islam Slimani aliyepo kwenye orodha ya wafungaji bora akiwa na mabao mawili amebainisha kuwa kikosi kizima
cha nchi hiyo kinatarajiwa kutoa msaada wa posho zao kwa watu wa
Gaza.
Timu ilirejea nyumbani wakiwa mashujaa na wachezaji wameamua kutoa
posho zao kwa wale ambao wanazihitaji zaidi, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa miongoni mwa Ibada ndani ya Uislam.
Hatua hiyo ya Algeria
imekuja huku wawakilishi wengine wa Afrika katika michuano hiyo kama
Ghana, Nigeria na Cameroon kukumbwa na msuguano katika kambi zao
kutokana na posho hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuenguliwa
mapema.
Algeria ni nchi ya Kiislam iliyopo Kaskazini mwa Afrika na inaelezwa kufungwa kwa mabao 2-1 katika hatua ya lala salama na Ujerumani ilitokana na swaumu.
No comments:
Post a Comment