STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, July 4, 2014

Salvatory Ntebe amfananisha Oloba na Arsene Wenger

Ntebe alipokuwa akiwajibika uwanjani akiwa na Mtibwa
BEKI mpya wa timu ya Ruvu Shooting, Salvatory Ntebe amemmwagia sifa kocha wa timu hiyo Mkenya Tom Olaba akimfananisha na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger.
Ntebe aliyetua Ruvu akitokea Mtibwa alisema kwa jinsi Olaba alivyo mahiri katika ufundishaji na kuwa mlezi kwa wachezaji anamfananisha na Wenger anavyowaleta wachezaji Arsenal.
Beki huyo wa kati alisema Olaba anajua kukaa na wachezaji na kuwasaidia kama watoto wake, mbali na uwezo mkubwa wa kufundisha soka kitu kinachompa faraja kubwa kuwa naye.
'Mashabiki watarajie mambo mazuri maana nimekuja kwa kocha bora na mlezi ninayemfananisha na Arsene Wenger. Kocha huyu ni Wenger wa Afrika Mashariki," alisema.
Ntebe aliwahi kunolewa na Oloba wakati kocha huyo akiifundisha Mtibwa Sugar kabla ya kurejea kwao Kenya na wanakutana tena Ruvu Shooting baada ya kusajiliwa hivi karibuni kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Beki huyo ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Oloba kwa msimu ujao wakitokea Mtibwa, wengine ni Yusuf Nguya, Juma Mpakala na nyota wa zamani wa Mtibwa aliyekuwa akicheza soka la kulipwa Burundi, Chagu Chagula.

No comments:

Post a Comment