STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 31, 2014

HUYU NDIYE MSHINDI WA TMT 2014


MSHIRIKI kutoka Mtwara, Mwanaafa Mwinzago ameibuka kidedea katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Katika shindano hilo ambalo washiriki 10 walikuwa wakizitolea macho Shilingi milioni 50, Mwanaafa aliweza kuzoa kura nyingi zaidi na hivyo kujiwekea kibindoni mamilioni hayo na kuwatimulia vumbi washiriki wengine.
Awali kabla ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotions, Johnson Lukaza alitoa ahadi kwamba kampuni hiyo itajitolea kumsomesha mtoto Mwanaafa ili aweze kufanikiwa kufikia malengo yake.
Mwanaafa ndiye mshiriki mdogo kuliko wote katika shindano hilo lililoandaliwa na Proin Promotions ambapo miongoni mwa majaji watatu, wawili walikuwa waigizaji maarufu nchini, Single Mtambalike ‘Ritchie Rich’ na Yvonne Cherie ‘Monalisa’. Jaji Mkuu alikuwa Roy Sarungi.
Mara baada ya kutangazwa mshindi, Mwanaafa aliangua kilio cha furaha kuonesha kutoamini kwamba amefanikiwa kunyakua mamilioni hayo huku akihaha huku na kule kumtafuta mama yake jukwaani.
Hata baada ya kuitwa na kukabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 50 na Mwenyekiti wa Proin Promotions, Mwanaafa aliendelea kububujikwa machozi ya furaha kuonesha kabisa kutoamini kinachotokea usiku huo.

No comments:

Post a Comment